Akitoa ufafanuzi huo jana jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo Bi. Janeth Ruzangi alikiri kuwepo kwa makampuni yanayofanya kazi ya ulinzi bandarini na akafafanua kuwa hayahusiki kwa namna yoyote ile kulinda sehemu za ndani za ofisi zilizoko bandarini.
“Ninapenda
kuwafahamisha wananchi kuwa Bandari inalindwa na walinzi wa aina tatu ;
Jeshi la polisi, Polisi wasaidizi walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari
Tanzania (Auxilliary Police) pamoja na walinzi wa Makampuni binafsi”
Aliongeza
kuwa makampuni hayo yanalinda maeneo ya nje ya bandari yakiwemo
maegesho ya magari ya watumishi wa mamlaka kama ilivyo kwenye ofisi
nyingine.
Aidha,alifafanua
kuwa Polisi wa bandari walioajiriwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania wako
kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na Bunge na wamepata baadhi ya
mafunzo ya kipolisi.
Ikumbukwe
kuwa agizo la kuwandoa walinzi wa makampuni binafsi kwenye maeneo nyeti
ya bandari lilitolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mwezi
Februari mwaka huu alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini hapo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment