WAZIRI
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Kassim Majaliwa
amesema Mkurugezi yeyote wa Halmashauri nchini atakayeshindwa kutenga
asilimia 10 ya mapato kwa ajili ya wanawake na vijana ataondolewa.
Amesema
suala la kila Halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake kwa ajili
ya kuwawezesha wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi na kuondokana na
utegemezi ni la lazima na si hiari.
Waziri
Mkuu, Majaliwa ameyasema hayo jana (10 Aprili, 2016) alipokuwa
anazungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Kitandi,
Mtimbo, Likunja, Nkowe na Namahema ambako alifanya mikutano ya hadhara.
“Halmashauri
ambayo itashindwa kutenga asilimia 10 kwa maana asilimia tano kwa
ajili ya vijana na tano kwa ajili ya akinamama Mkurugenzi wake atakuwa
anatafuta safariiri,” alisema Waziri Mkuu, Majaliwa.
Waziri
Mkuu, Majaliwa yupo wilayani Ruangwa, Lindi kwa ajili ya ziara ya
kikazi inayolenga kukagua shughuli za maendeleo, ambapo amewasisitiza
Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutimiza wajibu wao na serikali
haitamvumilia yeyote atakayeshindwa.
Pia
Waziri Mkuu, Majaliwa aliwataka wananchi hao kujiunga katika vikundi
vya uzalishaji mali ili zitakapofika sh milioni 50 za kila kijiji
zilizoahidiwa na Rais, Dk. John Magufuli waweze kunufaika.
Alisema
fedha hizo ambazo zitatolewa kuanzia mwezi Julai mwaka huu zitagawiwa
katika vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa na si kwa mtu mmoja mmoja
hivyo amewataka watendaji wa kata na vijiji kuwahamasisha wananchi
kujiunga katika vikundi.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu, Majaliwa alisema serikali imefuta tozo tano
kati ya tisa za zao la korosho zilizokuwa kero ya muda mrefu na kufanya
wakulima wachukie mfumo wa Stakabadhi ghalani.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment