Naibu
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amezima hoja ya Mbunge wa Nzega Mjini,
Hussein Bashe (CCM) aliyeomba suala la kupanda bei ya sukari lijadiliwe
bungeni.
Wakati
hayo yakitokea wananchi wa Mkoa wa Mbeya wameviomba vyombo vya dola
kupekua malori yanayotokea Malawi, kwa madai yanabeba sukari ya magendo
na kuingiza nchini.
Akitumia
kifungu cha Kanuni za Bunge cha 47(1, 2, 3), mbunge huyo alisema
bungeni mjini hapa jana, kuwa suala hilo ni muhimu kwa Watanzania hivyo
ni vyema likajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Alisema
tangu itangazwe utaratibu wa kusitisha sukari kuingizwa nchini kutoka
nje, bidhaa hiyo imekuwa adimu na bei yake imekuwa inapanda kila siku na
kusababisha maisha ya wananchi kuzidi kuwa magumu.
Hata
hivyo, kabla hajamalizia kuzungumza, Dk Ackson alimkatiza Bashe,
akisema suala hilo lilishafanyiwa kazi Alhamisi wiki iliyopita, wakati
wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
“Mtakumbuka
Waziri Mkuu Alhamisi ya wiki iliyopita, alitoa maelezo na akatoa
maelekezo kuwa sukari itaruhusiwa kuingizwa nchini kwa kiasi ambacho
alitaja,”alisema.
Alisema
pamoja na udharura wake kwasababu ilishatolewa maelekezo, wabunge
wasubiri yale maagizo ya Waziri Mkuu kuuliza kama sukari imeingia ama
haijaingia na kama hajaingia lini inaingia.
Wiki
iliyopita, Waziri Mkuu akijibu hoja iliyoibuliwa bungeni hapo inayohusu
pia bei ya sukari, Waziri Mkuu alisema serikali imeruhusu kiasi kidogo
cha sukari kuingizwa nchini ili kupunguza tatizo la upungufu wa bidhaa
hiyo.
Kwa
mujibu wa Majaliwa, Tanzania ina uwezo wa kuzalisha tani 300,000 za
sukari kwa mwaka wakati nchi inahitaji tani 420,000 hivyo kuwepo na
upungufu wa tani 120,000.
Aidha,
mapema mwezi uliopita, serikali ilitangaza kuwa bei elekezi ya sukari
itakuwa Sh 1,800 kwa kilo, lakini hali katika maeneo mbalimbali nchini
ni tofauti, kwani bidhaa hiyo muhimu inauzwa kwa bei ya juu.
Katika maeneo mbalimbali ukiwamo Mkoa wa Dar es Salaam, sukari inauzwa kuanzia Sh 2,200 hadi Sh 2,500 kwa kilo.
Baadhi
ya wafanyabiashara nchini wameamua kufanya njama za kuficha bidhaa hiyo
ili kuonekana kuwa kuna uhaba ili waruhusiwe kuagiza kutoka nje, jambo
ambalo limekwishakataliwa na Rais John Magufuli.
Wiki
iliyopita, mkoani Singida, wananchi walisaidia kukamatwa kwa mifuko 655
ya sukari sawa na tani 24.3, na kutiwa nguvuni wafanyabiashara wawili
pia wakihusishwa na bidhaa hiyo ambayo ilifichwa stoo.
Waliokamatwa
ni Mohamed Alute Ally (44) mfanyabiashara wa Unyankindi aliyekutwa na
mifuko 335 ya kilo 25 kila mmoja na Yusufu Suleiman (39) mfanyabiashara
wa Minga aliyepatikana na mifuko 320 ya kilo 50.
Taarifa
ya kukamatwa kwa sukari hiyo na wafanyabiashara hao ilitolewa na
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ambaye pia ni Mkuu
wa Wilaya ya Singida, Saidi Amanzi.
Taarifa
zilieleza kuwa mfuko mmoja wa sukari ambao huuzwa kwa Sh 92,650 sasa
unauzwa kati ya Sh 115,000 na Sh 120,000 huku kilo moja ikiuzwa kati ya
Sh 2,400 na 2,800 kwa kilo kinyume cha bei elekezi ya Sh 1,800.
Kutoka
Mbeya, wananchi jijini hapa wamevitaka vyombo vya dola kuyapekua malori
yanayotokea nchi jirani ya Malawi, kwa kile walichodai yanabeba sukari
ya magendo na kuingiza nchini.
Wakizungumza
kwa sharti la kutotajwa majina yao, walisema hivi karibuni kuna malori
manane ya kampuni moja yalibeba shehena ya sukari yakitokea Malawi na
yaliegesha kwenye moja ya kituo cha mafuta cha Uyole kwa lengo la
kutafuta wateja.
Mkazi
mwingine wa Mtaa wa Soweto, Hamphrey Lyoto alisema suala la uingizwaji
wa sukari, linafanywa mchana ambapo malori yanapeleka sukari kwenye
nyumba ya mfanyabiashara mmoja eneo hilo aliyejiwekea kiwanda cha kuweka
sukari kwenye mifuko ya kilo moja moja na nusu kilo.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula alipoulizwa juu la
suala hilo, alisema hafahamu lolote kwa kuwa ameanza kazi hivi karibuni,
lakini aliahidi kulifutalia.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment