WAZIRI
 Mkuu, Kassim Majaliwa amesisitiza kuwa ahadi zote zilizotolewa kipindi 
cha kampeni mwaka jana pamoja na zilizoko kwenye Ilani ya Chama Cha 
Mapinduzi (CCM), zitatekelezwa kama zilivyoahidiwa.
Pia
 amesisitiza kuwa kupitia ahadi hizo, wamedhamiria kutekeleza kwa 
vitendo ujenzi wa barabara zote kwa kiwango cha lami na kwa sasa 
wanatarajia kuanza na barabara zinazounganisha mikoa.
Kauli
 hiyo ilitolewa na kiongozi huyo bungeni Dodoma jana wakati akijibu 
swali la Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala (CCM) aliyebainisha kuwa 
katika moja ya ahadi zilizopo kwenye ilani ya CCM ni pamoja na ujenzi wa
 barabara kwa kiwango cha lami.
Mbunge
 huyo alihoji, je Serikali ya Awamu ya Tano imejipangaje katika 
kutekeleza ahadi hiyo? Akijibu swali hilo, Majaliwa alisema CCM kupitia 
ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2015, imebainisha ahadi mbalimbali 
ambazo chama hicho kimeamua zitekelezwe katika kipindi cha miaka mitano.
Alisema
 pamoja na ahadi ya ujenzi wa barabara katika kiwango cha lami, ahadi 
zote zilizomo kwenye ilani hiyo zitatekelezwa kama zilivyoahidiwa. 
“Ni
 kweli kwamba tumedhamiria kujenga barabara zetu kwa kiwango cha lami. 
Na tumeanza na mkakati wa kuunganisha barabara kwa ngazi ya mikoa, 
tukishakamilisha tunaingia kwenye barabara zinazounganisha wilaya,” alisema. 
Alisema
 pia barabara zote zilizoainishwa katika ilani hiyo ya CCM katika awamu 
hiyo ya tano, zitakamilishwa kupitia bajeti itakayopitishwa na Bunge 
hilo ya mwaka 2016/17.
“Naomba
 niwashawishi waheshimiwa wabunge muipitishe bajeti hii ili tuweze 
kukamilisha barabara ambazo mmezitaja sana humu ndani. Pale ambapo 
barabara za mikoa hazijakamilika tunataka tuzikamilishe,”alisema.
 TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]

0 comments:
Post a Comment