TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN
ameviagiza viwanda vyote nchini kutumia msibomilia (BARCODES) za
Tanzania kama hatua ya kuimarisha masoko na utambulisho wa bidhaa za
Tanzania katika masoko ya ndani na ya nje ya nchini.
Makamu
wa Rais ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa kampeni ya “NUNUA 620
Nunua Bidhaa za Tanzania” pamoja na Kusherekea miaka MITANO ya Taasisi
ya Global Standard One –GSI-kwenye Viwanja wa Mwalimu Nyerere katika
Maonyesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es salaam (SABASABA)
mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho.
Makamu
wa Rais amesema matumizi ya BARCODES ni muhimu na ni ya lazima kwa
sababu yanajumuisha taarifa nyingi ikiwemo asili ya bidhaa,jina la
kampuni, kumbukumbu za uzalishaji,utunzaji,usafirishaji na usambazaji wa
bidhaa.
Ameleeza
kwamba itakuwa ni aibu kubwa kama katika masoko ya ndani ya nchi bado
kutakuwa na bidhaa zinazotumia msibomilia (BARCODES) za nje na
kusisitiza kuwa matumizi ya Barcodes za Tanzania zitazuia na kupungua
upotevu wa ajira kwa wataalamu wa ndani ya nchi.
Makamu
wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema kuwa serikali ya awamu ya TANO ipo
Tayari kufanya kazi na sekta binafsi katika kuleta mapinduzi makubwa
yatakayosaidia kukuza uchumi wa taifa.
Kuhusu
uanzishwaji wa Majukwa ya kumwezesha wanawake Kiuchumi nchini, Makamu
wa Rais amesema kuwa atahakikisha majukwaa hayo yanaleta matokeo chanya
na yenye tija kwa wanawake Wakitanzania mijini na viijijini kwa
kuwezeshwa kupata kupata elimu ya ujasiriamali,fursa za
masoko,upatikanaji wa mikopo nafuu pamoja na elimu ya kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazowakwaza wanawake kiuchumi.
Makamu
wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanawake kote nchini kujiunga na
majukwaa hayo pindi yatakapoanzishwa kwenye maeneo yao kwa sababu
yatakuwa na faida kubwa kwao kwa kuunganisha nguvukazi zao na kuzalisha
bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.
Imetolewa na
Ofisi ya Makumu wa Rais
2-Jul-16
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment