Serikali
ya Iraq imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia maafa
yaliyotokwea kutokana na shambulio la bomu ambalo limeua watu wapatao
mia 120 katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Baghadad.
Katika shambujlio hilo watu 150
walijeruhiwa vibaya wakati lori lililokuwa na milipuko lilipolipuka
nyakati za usiku karibu na msikiti katika wilaya ya Karanda.
Mlipuko huo uliotokea katika eneo lenye
shughuli nyingi ambapo baadhi ya watu walikkuwa wakijipatia mahitaji kwa
ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Tayari wapiginaji wa Islamic State
wamekiri kuhusika na mlipuko huo.Muda mfupi baada ya mlipuko huo Mkuu wa
majeshi ya nchi hiyo Major Generali Kadimu Shabaani alifika katika eneo
la tukio.”
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment