Uganda Yaitoa Kimasomso Afrika Mashariki... Yafuzu AFCON 2017 Kwa Mara Ya Kwanza Tangu 1978


Timu ya taifa Uganda imefuzu katika fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika 2017 baada ya miaka 38, The Cranes walishinda 1-0 dhidi ya Comoro siku ya Jumapili, ushindi ambao umewafanya kutimiza pointi 13 zilitosha kuwapa tiketi ya AFCON 2017.

Goli la Uganda limefungwa na Farouk Miya mbele ya mashabiki kibao wa Uganda jijini Kampala.
Mara ya mwisho The Cranes kucheza Afcon ilikuwa mwaka 1978 ilipofanikiwa kufika hadi fainali na kufungwa na Black Stars ya Ghana.

Mataifa 16 yatashiriki michuano hiyo itakayoandaliwa 14 Januari hadi 5 Februari. huko Nchini Gabon.
Timu zilizofuzu mpaka sasa. #AFCON2017
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment