Kambi rasmi ya upinzani
imepanga kufanya vikao vya kujadili suluhu ya kudumu ya mgogoro na Naibu
Spika, Dk Tulia Ackson uliosababisha wabunge wanaounda Ukawa kususia
vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo.
Vikao hivyo vinapangwa kufanyika wakati mkutano wa nne ukianza rasmi kesho, baada ya kuahirishwa mwishoni mwa Juni mwaka huu wakati wa mkutano wa Bajeti.
Vikao hivyo vinapangwa kufanyika wakati mkutano wa nne ukianza rasmi kesho, baada ya kuahirishwa mwishoni mwa Juni mwaka huu wakati wa mkutano wa Bajeti.
Mbunge wa Vunjo
(NCCR- Mageuzi), James Mbatia alieleza jana kuwa uamuzi wa kufanya
vikao hivyo umefikiwa baada ya upinzani kukaa kikao na viongozi wa dini
Agosti 24 mwaka huu ili kutafuta suluhu ya kudumu.
“Kikao cha kwanza
tutakaa kamati ya uongozi ya wabunge wa upinzani kujadili suala hilo na
baadaye tutamaliza na kikao cha wabunge wote ili kubaini njia endelevu
za kumaliza jambo hilo,” alisema Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi.
Wabunge wa Ukawa wamekuwa wakisusia vikao vinavyoendeshwa
na Naibu Spika kwa madai ya kutoridhishwa na uongozi wake tangu Mei
mwaka huu, baada ya Dk Tulia kukataa kujadili hoja ya kufukuzwa
wanafunzi zaidi ya 8,000 stashahada ya ualimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma
(Udom).
Hata wakati wakisubiri kufanyika vikao hivyo ambavyo Mbatia
hakutaka kuelezea kwa undani, upinzani ulitangaza kurudi bungeni baada
ya mkutano wao na viongozi wa dini.
Katika mkutano na wanahabari Agosti
25, Mbatia kwa niaba ya vyama vilivyoshiriki mkutano huo wakiwamo
ACT-Wazalendo, alisema wangejadiliana namna ya kufanikisha jambo hilo
kama sehemu ya kutii ushauri wa viongozi hao wa kiroho.
Hata hivyo,
haijawekwa bayana iwapo kesho Ukawa wataendelea na vikao hata kama Dk
Tulia ataendelea kuongoza kiti hicho ama la.
Mbatia alisema jana kuwa watatoa taarifa rasmi leo namna vikao hivyo vitakavyofanyika na siku husika.
Mbatia alisema jana kuwa watatoa taarifa rasmi leo namna vikao hivyo vitakavyofanyika na siku husika.
Kuhusu kupata taarifa ya mwenendo wa mchakato wa kutafuta
maridhiano ulioelezwa na Spika Job Ndugai hivi karibuni, Mbatia alisema
hawajapata chochote na wao wanasikia kwenye vyombo vya habari kama
wengine.
Alipoulizwa ni lini vikao vya maridhiano kati ya pande hizo
yataanza, Ofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya
alisema Spika anatarajiwa kufika ofisini leo na kwamba kama ataona kuna
haja ya kufanya hivyo atapanga utaratibu wa namna anavyoona inafaa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment