Kudura Kiboka anayedaiwa kuwa kinara wizi wa bodaboda
Stori: Mwandishi Wetu, Wikienda
Dar es Salaam: Hapa kazi tu! Jamaa anayedaiwa kuwa kinara wa wizi wa
bodaboda jijini Dar na kuzua hofu kwa waendesha pikipiki, Kudura Kiboka,
mkazi wa Buguruni, amenaswa kisha kufanikisha kukamatwa kwa jamaa
aliyetajwa kuwa mfadhili wake aitwaye Massawe almaarufu Mwarabu.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni baada ya waendesha bodaboda wanne
ambao ni wakazi wa Mbezi ya Kimara na Mbagala jijini Dar, kumripoti
Kudura polisi kuwa ni mtu hatari ambaye likitajwa jina lake kwa
waendesha bodaboda wanashtuka.
Waendesha bodaboda hao waliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, baada ya
Kudura kukamatwa na kumtaja Mwarabu ndipo waendesha bodaboda
wakaunganisha nguvu na kumsaka mfadhili huyo aliyesemekana hayupo jijini
Dar.
Masawe anayedaiwa kumfadhili kudura katika wizi huo.
Jamaa hao walidai walifanikiwa kushirikiana na polisi kumsaka Mwarabu ambaye alifikishwa Kituo cha Polisi cha Tabata-Bima, Dar.
Mtu wa kwanza kuporwa bodaboda, Abdallah Hemedi, mkazi wa Mbagala
alidai kuibiwa pikipiki yake baada ya kukodiwa na Kudura kutoka Mbagala
hadi Kawe kisha Mlimani City na Tabata-Bima ambapo waliingia ndani ya
nyumba moja kwa lengo la kumtafuta mwenye nyumba huku wakiacha bodaboda
nje ndipo Kudura alipotoroka na pikipiki akimuacha dereva ndani ya
nyumba hiyo.
Baada ya kutapeliwa, jamaa huyo alitoa taarifa katika Kituo cha
Polisi cha Tabata-Bima na kupewa RB namba TBT/RB/3270/2015 na
TBT/IR/1742/2015- WIZI WA PIKIPIKI ambazo pia ndizo zilizotumika
kumkamata Mwarabu.
Masawe akiwa mikononi mwa dola.
MWATHIRIKA WA PILI
Deusdediti Mrandu, mkazi wa Mbezi-Luis, yeye alidai kuibiwa bodaboda Januari, mwaka huu na huyohuyo Kudura mara baada ya kumlaghai kisha kutoroka na pikipiki yake ambapo alitoa taarifa Kituo cha Polisi cha Kimara na kupewa RB namba KMR/RB2887/2016 -WIZI WA PIKIPIKI.

MWATHIRIKIA WA TATU
Mjane aliyefahamika kwa jina la Tatu Shabban au Mama Tashi, mkazi wa Mbezi ya Kimara, naye alidai
kuibiwa pikipiki yake na Kudura, Januari, mwaka huu ambapo alifungua jalada la kesi kwenye Kituo cha
Mbezi-Kwayusuf na kupewa RB namba KMR/RB/246/2016- WIZI WA PIKIPIKI.
kuibiwa pikipiki yake na Kudura, Januari, mwaka huu ambapo alifungua jalada la kesi kwenye Kituo cha
Mbezi-Kwayusuf na kupewa RB namba KMR/RB/246/2016- WIZI WA PIKIPIKI.
Baadhi ya RB anazotuhumiwa Kudura.
MWATHIRIKA WA NNE
Dereva mwingine aliyefahamika kwa jina la Ahadi Senkunde kutoka Buguruni alidai kukodiwa kwenda Mabibo-Mwembeni na mtu aliyemtaja kwa jina la Kudura ambapo walipofika sehemu alimnywesha viroba, alipozinduka ulikuwa usiku wa saa 6:00 na kukuta jamaa alishatokomea na bodaboda yake ndipo akatoa taarifa polisi na kupewa RB namba KMR/RB2887/2016- WIZI WA PIKIPIKI.

KAKA MTU AMKAMATISHA
Ilidaiwa kuwa, kutokana na matukio ya Kudura huku kesi zote zikipelekwa
kwa kaka yake, Kiboka Kiboka, kaka mtu alichoka ndipo akamkamatisha kwa
wanaodai kuporwa bodaboda kisha akatiwa mbaroni.
KAMANDA KINONDONI
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime alisema hana taarifa za kukamatwa kwa mtu huyo lakini zitakapomfikia atazifanyia kazi.
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime alisema hana taarifa za kukamatwa kwa mtu huyo lakini zitakapomfikia atazifanyia kazi.
KAMANDA ILALA
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Lucas Mkondya
alisema analifuatilia suala hilo akianzia kwenye Kituo cha Polisi cha
Tabata-Bima hivyo atatoa taarifa baada ya kupata maelezo
yanayojitosheleza.
-Via GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment