Mchezo huo utafanyika Aprili 9, mwaka huu, Uwanja wa Taifa uliopo Wilaya ya Temeke Dar es Salaam, kisha zitarudiana wiki mbili baadaye mjini Cairo, Misri.Pluijm amesema sababu ya kuandaa mikakati hiyo ni kutokana na ubora na uzoefu waliokuwa nao Al Ahly ambao kwa sasa wanafundishwa na Mholanzi mwenzake Martin Jol, aliyewahi kuzifundisha timu za Tottenham na Fulham zinazoshiriki Ligi Kuu ya England.
“Huu ni mchezo mkubwa na tunakutana na timu yenye rekodi nzuri Afrika na wachezaji na kocha mwenye uzoefu mkubwa, hivyo ni vyema tukajipanga kwa kuwa na mbinu nyingi za kivita,” alisema.
Alisema anachotaka ni kuona timu yake inapata ushindi wa mabao yasiyopungua matatu nyumbani ili waweze kuwa na kazi nyepesi ya kulinda ushindi wao mchezo wa marudiano.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment