Kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho imeripotiwa kuwa yuko mbioni kujiunga na klabu ya Manchester United baada ya msimu kuisha na atakuwa kocha ambae atalipwa hela nyingi kuliko makocha wote duniani imeripotiwa na gazeti la Express kuwa paundi milioni 60 ndio thamani ya kocha huyu wa kireno.
Jose Mourinho mara nyingi hatulii sehemu moja kutokana na kutaka matokeo zaidi na mafanikio pasipo kutengeneneza timu inasemekana kocha huyo pindi atuaapo manchester united ana taratibu ya kuja na wachezaji wake ambapo tushawahi kuona timu nyingi alizopitia.
Baada ya kurejea Chelsea aliwaondoa Juan Mata na Kevin Debruny na kuwa chukua Zuma,Andrie Schurrle pamoja na Roicy Remmy.
Vyombo mbalimbali vya habari vina ripoti kuwa moja ya chaguo lake ni Harry Kane wa Totenhham pamoja na Rafael Verane kutoka Madrid na kuna wachezaji wataondoka klabuni hapo kwa ajili ya kuwapisha wachezaji ambao kocha huyo ata wahitaji.
Mashabiki wa Manchester United kwa sasa hawataki mpira mzuri wanataka matokeo kulingana na kauli zao wenyewe wana bariki ujio wa Mourinho kwani wanaamini kuwa ataweza kuleta mapinduzi ya kukosa ubingwa wa EPL na kukosa michuano mikubwa ambapo timu hiyo haijapata matokeo mazuri tangu Alex furgason astafu mwaka 2012.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment