Na Albogast Benjamin
Hakuna Manchester wala Chelsea tena hakuna Arsenal wala Liverpool mbaya zaidi hakuna Manchester City pia kwenye jeshi hili jipya la Uingereza na kama ndio hiki walichokifanya hawa wachezaji kutoka vilabu vinavyoongoza ligi kwa nafasi mbili za juu ni bayana kuwa hawajabahatisha kuwepo pale juu, Kwa lugha sanifu tunasema Hakuna Janja Janja ni soka la kueleweka ndio litakupa matokeo.

England iliyoonekana kuwa nchi ya kinyonge linapokuja suala la timu ya taifa na michuano ya kimataifa huenda sasa kupitia wachezaji wa vilabu hivi viwili Leicester na Tottenham ikapata nafuu na ikajisogeza pazuri kama inavyostahili kutokana na uwekezaji mkubwa kwenye soka haswa ligi yao maarufu ya EPL.
Jana usiku ilichezwa mechi ya kirafiki kati ya Ujerumani waliokuwa nyumbani kuwaarika timu ya taifa ya Uingereza na mchezo ulimalizika kwa England kushinda bao 3 kwa moja licha ya wenyeji kuanza kufunga kipindi cha kwanza kisha kuongeza bao la pili mapema kipindi cha pili, England ikiongozwa na safu ya washambuliaji wawili wanaotoka kwenye vilabu vinavyoshika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi iliweza kurudisha mabao hayo na hatimaye kuongeza bao la tatu na la ushindi.
Watungaji wa mchezo huo Upande wa Ujerumani walikuwa ni Toni Kroos dk43 na Mario Gomez dk57 wakati mabao ya England yakifungwa na Harry Kane dk61, Jamie Vardy dk74 na Eric Dier dk90 bao ambalo lilimsababishia kuumia kutokana na mazingira magumu ya kufunga kwa kichwa. Timu hizi zimekutana mara 34 Ujerumani wakishinda michezo 14 huku Uingereza wakishinda michezo 16 na kutoka sare michezo 4.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment