Mwandishi Bi. Salma Said.
TAARIFA KWA UMMA
KUTOWEKA KWA MWANDISHI SALMA SAID
Kampuni ya Mwananchi Communications Limited
(MCL), wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na
MwanaSpoti, inaendelea kufuatilia kwa makini kutoweka kwa Mwandishi wetu
wa Zanzibar, Bi Salma Said.
Taarifa za kutoweka kwa Bi Salma
zilitufikia Ijumaa mchana tarehe 18 Machi 2016 kupitia kwa mume wake.
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote inayoonyesha ni nani au chombo gani
kinamshikilia au kumhifadhi.
Hali hii inatutia wasiwasi mkubwa kama
kampuni na wadau wa habari. Tunachukua fursa hii kuvitaka vyombo vya
dola – vyenye dhamana ya ulinzi na usalama wa raia wake – kulitafutia
ufumbuzi wa haraka suala hili ili kumaliza utata uliozingira kutoweka
kwa Mwandishi Salma.
Imetolewa na
Francis M. Nanai
Mkurugenzi Mtendaji,
Mwananchi Communications Ltd
20.03.2016
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment