23 PICHAZ: Tazama Treni 11 za Kifahari Zaidi Duniani, Moja Ilishawahi Kuja Tanzania


Kuna baadhi ya watu wangu wa nguvu ambao wanapenda kusafiri kwa aina fulani ya vyombo vya usafiri kwa ajili ya mapumziko na kutalii sehemu mbalimbali, April 7 2016 kupitia tovuti ya chombo cha habari cha Marekani ‘CNN’ wametoa list ya treni 11 za kifahari zaidi duniani, moja ya treni hizo ilifika Tanzania kwa ajili ya shughuli za utalii.

Treni ya Rovos rail ambayo hutembea polepole na kuelekea maeneo mbalimbali ya vivutio vya nchi za Afrika kama vile Afrika kusini, Zimbabwe, Namibia na Tanzania. Rovos rail ni treni ya kifahari zaidi ambayo hufanya safari ndefu kwa siku kadhaa usiku na mchana kwa sababu treni hiyo kamwe haisafiri zaidi ya kilometa 60 kwa saa, kwenye treni hiyo abiria wanaweza kufungua madirisha nakupata hewa safi au kupiga picha.
UNAWEZA KUANGALIA MOJA YA SAFARI ZA TRENI YA ROVOS RAIL KUTOKA CAPE TOWN HADI DAR ES SALAAM.

Treni ya Rovos Rail


Treni ya Rovos rail sehemu ya ndani
Nimekuwekea picha ya treni nyingine 10 ambazo zinafanya safari za kifahari zaidi maeneo mbalimbali duniani.
Seven star, ni treni ya kifahari zaidi Japan ambayo ina mabehewa saba ambayo yanachukua watu 30 kwenye siti 14.


2. Rocky Mountalneer, treni ya Canada ambayo hufanya safari mbalimbali Vancouver


Treni ya Rocky Mountalneer sehemu ya ndani
3. Maharajas’ Express- India


Treni ya Maharajas’ Express sehemu ya ndani
4. Golden Egle inafanya safari kutoka Moscow kwenda Vladivostock


Sehemu ya chakula kwenye treni ya Golden Egle
5. Belmond Royal Scotsman inafanya safari mbalimbali UK ambapo inachukua watu 39 ikiwa ni kiwango cha juu kabisa



6. Blue Train, hii hufanya safari za Pretoria-Cape town South Africa


sehemu ya ndani
7. Venice Simplon-Orlent-Express, hufanya safari kwenye maeneo mbalimbali ya ulaya



8. The Ghan, hufanya safari zake kutoka Darwin kwenda Adelaide ambayo hupitia katikati ya Australia


Mgahawa unaopatikana ndani ya treni ya Ghan
9. Treni ya Canadlan, hufanya safari zake za Toronto na Vancouver


Sehemu ya kulala inayopatikana ndani ya treni ya Canadian
10. Treni ya Transcantabrico Grain Lujo, hii ni moja ya treni za kifahari zaidi kaskazini mwa Hispania

TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment