TANZIA: MBUNGE CHRISTINA MUGHWAI LISSU WA CHADEMA AFARIKI DUNIA LEO APRIL 7

Christina Mughwai Lissu enzi za uhai wake.
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoani Singida, Christina Mughwai Lissu (CHADEMA) amefariki dunia leo kwa ugonjwa wa kansa. Alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Aghakhan jijini Dar es Salaam.
Marehemu Christina ni dada wa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Mhe. Tundu Lissu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMEN

Hapo chini ni ujumbe wa Tundu Lissu kuhusu taarifa hiyo
“Waheshimiwa nawasalimu kutoka Kibondo. Nina habari zisizokuwa njema. Dada yangu na aliyekuwa Mbunge wetu wa Viti Maalu m Mh. Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya Aga Khan Dar. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa cancer tangu mwaka jana. Kwa niko nje ya Dar na ndio kwanza taarifa hizi zimenifikia, sina taarifa zaidi juu ya mipango ya mazishi, etc. Tutawataarifu baada ya familia kuwa tumeshauriana”
-Tundu Lissu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment