Ama
kwa hakika usemi wa “mfupa uliomshinda fisi, Mbwa hauwezi”, Kocha wa
zamani wa Dar es salaam Young Africans ambae alikuja kwa mbwembwe nyingi
mwisho akashindwa kuendana na kasi ya timu hiyo ametupiwa virago na
Timu ya Taifa ya Togo.
Thom
Santfiet aliwahi kuifundisha Yanga kabla kutimuliwa na baadae kupata
kibarua nchini Togo kukinoa kikosi hicho, nako pia ametimuliwa kwa kile
kilichodaiwa kuwa mwenendo wa timu hiyo kutoridhisha hasa katika
kuelekea Afcon ambapo kwasasa Togo inashika nafasi ya Tatu katika kundi
lake.
Shirikisho
la chama cha soka nchini humo limeamua kumuajiri Mfaransa Cloude Leroy
kuionoa upya Togo kwa kumsainisha mkataba wa miaka mitatu kuifundisha
timu hiyo., kocha huyo mwenye historia nzuri Barani Afrika ambaye
ameishi kwa zaidi ya miaka 30, alishawahi kutunukiwa taji la Afcon akiwa
na Mwalimu wa kikosi cha Cameroon, pia ameshiriki mashindano hayo kwa
miaka 8.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment