RC SHINYANGA AKATAZA WATUMISHI WA UMMA KUNYANYASA WANANCHI

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango amewataka watendaji wa Serikali mkoani humu kuacha tabia ya kunyanyasa wananchi katika maeneo yao hasa pale wanapowaeleza kero zao.
Alitoa onyo hilo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga kwa lengo la kujitambulisha kwa wananchi na kueleza mikakati mbalimbali aliyoiandaa kuwaleta maendeleo.

Aliwatahadharisha watendaji wa Serikali wenye tabia hiyo ya kunyanyasa wananchi kuacha mara moja ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Alitaja mfano wa unyanyasaji huo kuwa ni pamoja na kutowasikiliza wananchi wanapokuwa na kero mbalimbali zinazotakiwa kutatuliwa na watendaji hao, kuwatolea lugha chafu pindi wanapofuata huduma katika ofisi za watendaji hao pamoja na kuwapuuza.
“Nataka watumishi wa Serikali walio chini yangu wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Wakurugenzi na wengine wote wenye tabia ya kunyanyasa wananchi kuiacha kuanzia leo,” alisema.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment