Baada ya klabu ya Simba kukaa kileleni kwa muda kwa kuwazidi michezo watani zao wa jadi Dar es Salaam Young Africans, April 16 Yanga walirejea kileleni baada ya kumaliza michezo yao ya viporo, lakini Simba walikuwa wanapewa nafasi ya kurudi tena kileleni leo April 17 2016 kama wangeshinda mchezo wao dhidi ya Toto Africans.
Kwa bahati mbaya leo April 17 uwanja wa Taifa Dar es Salaam Simba wamekubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Toto Africans na kuendeleza rekodi yao ya kusumbuliwa na Toto kila mara wanapokutana. Simba kabla ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu walikuwa na rekodi ya kushinda mechi zaidi ya 6 mfululizo baada ya kufungwa na Yanga mzunguko wa pili.
Toto Africans waliifunga Simba dakika ya 21 kupitia kwa kupitia kwa mshambuliaji wao Waziri Junior ambaye alitumia umahiri mkubwa wa kupokea mpira na kuuweka kifuani halafu kupiga shuti nje ya 18 na kumshinda golikipa wa Simba Vicent Agban.

-via millardayo
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment