Balozi Seif aliyasema hayo katika sherehe za ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la Polisi ngazi ya Koplo, Sajini na Staff Sajini yaliyofanyika kwenye Viwanja ya Polisi Ziwani mjini Zanzibar. Alisema kuyatumia mafunzo hayo vizuri katika utendaji wa kazi itawezesha kupunguza uhalifu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
“Nategemea mtabadilika na kuwa watendaji wazuri wanaochukia rushwa, kesi zitaendeshwa kwa haraka, haki itatendeka katika kutekeleza majukumu na haki za binadamu zitazingatiwa kwa lengo la kujenga heshima ya Serikali na kuleta uhusiano wa karibu baina yenu na wananchi,” alisema Balozi Seif.
Aidha, alilitaka Jeshi la Polisi kutopuuza uhalifu mdogo mdogo kwani uhalifu huo hatimaye husababisha uhalifu mkubwa na kusababisha uvunjifu wa amani katika nchi.
Naye Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame aliwakumbusha wahitimu hao kuwa wana wajibu mkubwa wa kuwalinda raia na mali zao pamoja na kulinda sheria za nchi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment