MAKAMU
wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo atawasha Mwenge wa Uhuru na kuzindua
rasmi mbio zake ili kukimbizwa katika halmashauri za wilaya na Manispaa
zipatazo 179 za mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Uzinduzi
huo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambao
utatanguliwa na shamrashamra za halaiki kutoka kwa vijana zaidi ya 1,000
na vikundi vya utamaduni kutoka wilaya za Morogoro na nje ya mkoa huo.
Katika
uzinduzi huo, viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na vyama vya siasa
wamealikwa kushiriki wakiwemo pia mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Miongoni
mwa mawaziri ambao hadi jana walikuwa tayari wamewasili mkoani hapa ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge, Sera,
Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji
Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mouldine
Castico.
Mawaziri
hao jana waliungana na Makamu wa Rais kutembelea mradi wa vijana
wajasiriamali wa mafundi seremala eneo la Mtaa wa Betero, Kata ya
Sabasaba, Manispaa ya Morogoro. Kaulimbiu za Mwenge wa Uhuru mwaka huu
ni “Vijana ni Nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na Kuwezeshwa.”
Baada
ya kuwashwa leo, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro na kuhitimishwa wilayani Gairo ambako Aprili 25,
mwaka huu utakabidhiwa mpakani mwa wilaya hiyo na Kilindi ya Mkoa wa
Tanga ili kuendelea na mbio zake.
Kwa
mujibu wa ratiba ya mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu, utakimbizwa
katika Halmashauri na Manispaa zipatazo 179 na kilele cha mbio hizo ni
Oktoba 14, mwaka huu katika Mkoa wa Simiyu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment