DEREVA teksi katika Manispaa ya Iringa, Elain Mahenge (27), anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mteja wake.
Mahenge,
Mkazi wa Semtema, Kihesa katika Manispaa ya Iringa, anadaiwa alikutwa
akifanya kitendo hicho dhidi ya mteja wake saa 3:45 usiku.
Kitendo
hicho cha ubakaji kimetokea ikiwa imepita takriban miezi miwili, tangu
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Iringa, kutoa elimu kwa
wananchi wa Kihesa juu ya kuwafichua watu wanaodaiwa kufanya vitendo vya
ubakaji.
Elimu
hiyo ilitolewa kutokana na kuripotiwa kukithiri kwa vitendo hivyo,
ikiwamo dhidi ya watoto wa kike na kuwalawiti watoto wa kiume, huku
zaidi ya watu 10 wakiwa wameshakamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za
kujihusisha na unyama huo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba, alisema jana kuwa tukio
hilo lilitokea Jumapili iliyopita, katika eneo la Kihesa. Alisema
mtuhumiwa alikutwa akimbaka mteja wake huyo, ambaye ni mkazi wa Mgololo,
Mufindi mkoani Iringa.
Kakamba
alisema mteja huyo alimkodi dereva huyo, baada ya kushuka kwenye gari
katika kituo kikuu cha mabasi cha Iringa na kumtaka ampeleke kwenye
nyumba ya kulala wageni iliyoko Kihesa.
“Inadaiwa
dereva teksi huyo alimchukua stendi hapo na kwenda alikoambiwa ampeleke
lakini alipofika njiani kwenye giza alisimama na kisha kumbaka binti
huyo,” alisema.
Kamanda
Kakamba alisema wakati dereva huyo akiendelea kufanya kitendo hicho,
binti huyo alipiga kelele ambazo zilisikika na askari polisi ambao
waliokuwa doria usiku huo na wakati polisi wanafika eneo la tukio tayari
mtuhumiwa alikuwa ameshamaliza kufanya kitendo hicho na ndipo
walipomkamata.
Alisema
kuwa mtuhumiwa yuko polisi na ushahidi umeonekana pale pale kwa kuwa
mazingira na hali waliyokutwa nayo dereva na binti huyo, yalidhihirisha
mtuhumiwa alitenda jambo hilo bila ya huruma tena kwa mteja wake, hivyo
mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakani wakati wowote kuanzia sasa.
Aidha
kamanda huyo aliwataka wakazi wa mji wa Iringa na viunga vyake kupanda
teksi ambazo zimesajiliwa na si kupanda teksi bubu kama aliyokuwa
ameipanda msichana aliyefanyikwa unyama huo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment