Wibert Molandi
YANGA imekubali kiroho safi kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini imewapoza mashabiki wake kwa kusema wasijali nguvu zote sasa zipo katika Kombe la Shirikisho Afrika, Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

Naodha wa timu ya Young Africans Nadir Haroub “Cannavaro.
Katikati ya wiki hii, Yanga iliondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa
Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly kwenye Uwanja wa Borg El
Arab mjini Alexandria huko Misri. Imetolewa kwa jumla ya mabao 3-2,
kwani awali ilitoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm,
alisema wametolewa na Al Ahly ambayo ni timu bora Afrika yenye nyota
saba wanaoichezea timu ya Taifa ya Misri na akawapongeza wachezaji wake
kwa ushindani waliouonyesha kwenye mechi hiyo.
Pluijm aliwapoza mashabiki wa Yanga kwa kusema: “Kasi tuliyotoka nayo
Misri tumepanga kuiendeleza kwenye ligi kuu na Kombe la FA ili kubeba
mataji hayo.
“Pia hatutazubaa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, mikakati tuliyoipanga kwenye timu ni kuchukua mataji yote ya michuano tunayoshiriki kwa kuanzia na ligi kuu na FA.
“Pia hatutazubaa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, mikakati tuliyoipanga kwenye timu ni kuchukua mataji yote ya michuano tunayoshiriki kwa kuanzia na ligi kuu na FA.
“Niongee ukweli, tumetolewa na timu bora Afrika yenye wachezaji wengi
wenye uzoefu wa kucheza michuano hiyo, hivyo naomba nichukue nafasi hii
kuwapongeza wachezaji wangu.
“Mashabiki watulie na wawe karibu nasi kuelekea mafanikio, hatutawaangusha, tutapambana hadi mwisho.”
Yanga kesho Jumapili inacheza na Coastal Union ya Tanga mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Mkwakwani, ambapo Pluijm alisema: “Tumejipanga kufanya vizuri ili tufike mbali.”

TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment