Ugomvi wa Kessy Wahamia YANGA SC, Azam FC

Hassan-‘-Kessy’-Ramadhani2
Hassan Kessy.
Wilbert Molandi,Dar es Salaam
SIKU chache baada ya Hassan Kessy kusimamishwa na uongozi wa Simba, meneja wa nyota huyo, Athumani Tippo ametamka kuwa timu itakayotoa dau nono ndiyo itakayonasa saini ya beki huyo.

Yanga na Azam FC ndiyo timu zinazotajwa kuwania saini ya beki huyo anayetarajiwa kumaliza mkataba wake mwezi ujao baada ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2015/16 kumalizika.

Kessy mapema wiki hii alisimamishwa na uongozi wa Simba kwa kosa la kumchezea rafu mshambuliaji wa Toto Africans, Edward Christopher na kusababisha atolewe nje kwa kadi nyekundu katika mchezo ulioisha kwa Toto kushinda bao 1-0.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Tippo alisema hajafuraishwa na kitendo cha mchezaji wake kufungiwa ambacho kinalenga kumuharibia kwenye klabu nyingine zilizovutiwa na huduma ya mteja wake.

Alisema wakati Simba wakitangaza kumsimamisha, tayari baadhi ya klabu zimeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili beki huyo aliyewahi kuichezea Taifa Stars na Mtibwa Sugar.
“Nisingependa kuziorodhesha klabu nilizofanya nazo mazungumzo katika kipindi hichi, cha kwanza tusubirie haya matatizo yamalizike kati yake na Simba ndiyo niweke kila kitu wazi,” alisema Tippo.
Hata hivyo, gazeti hili linafahamu kuwa mpango uliopo sasa ni Kessy kwenda ama Yanga au Azam ambazo zote zinamuwania kwa kasi.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment