REKODI YA YANGA SC KWA MICHEZO YAKE NA VILABU VYA NCHI ZA KIARABU HII HAPA

Dar es salaam Young Afrika ni miongoni mwa timu kongwe barani Afrika na ndio timu iliyochukua vikombe vya ligi kuu ya Tanzania mara nyingi ikiwa imechukua mara 25 lakini kwenye michuano ya kimataifa haina rekodi nzuri Baada ya kutupwa nje ya michuano ya klabu bingwa Afrika katika miaka tofauti iliyoshiriki pasipo kufika hatua za mbali.

Kuelekea mchezo wake na Al Ahly kesho April 9, jijini Dar es salaam tunakukumbusha mambo mbalimbali ya timu ya Yanga kwenye michuano ya kimataifa.
2008 – kombe la shirikisho
Libya: Al Akhdar 1-1 Yanga
Dar: Yanga 0-1 Al Akhdar ,
2009-Ligi ya Mabingwa
Tunisia: Esperance 3-0 Yanga
Dar: Yanga 0-1 Esperance

2011- Ligi ya Mabingwa
Cairo: Al Ahly 3-0 Yanga
Dar: Yanga 0-1 Al Ahly
2012-kombe la shirikisho
Dar: Yanga 1-1 Zamalek
Misri: Zamalek 1-0 Yanga
2014- Ligi ya Mabingwa
Dar: Yanga 1-0 Al Ahly
Cairo: Al Ahly 1-0 Yanga
Yanga ilitolewa kwa mikwaju ya Penati (6-5)
2015- Kombe la shirikisho
Dar: Yanga 1-1 Sahel
Tunisia: Sahel 1-0 Yanga
Ni baadhi tu ya mechi za Yanga dhidi ya timu zinazotoka nchi za kiarabu ambapo imekuwa ni vigumu kushinda hivyo tusubiri mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment