WAZIRI MAGHEMBE APOKEA MSAADA WA NDEGE KUTOKA UJERUMANI

SERIKALI ya Ujerumani imetoa msaada wa ndege maalumu aina ya “Husky A-1C Aircraft” kwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Malisili na Utalii kusaidia katika doria za kupambana na ujangili katika Pori la Akiba la Selous.

 Msaada huo wenye thamani ya Euro 200,000 sawa na Sh milioni 498.2 umekabidhiwa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na Waziri wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo wa Serikali ya Shirikisho la Ujerumani, Dk Gerd Muller katika hafla fupi iliyofanyika Matambwe ndani ya Pori la Akiba la Selous.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na maofisa wa Ubalozi wa Ujerumani nchini wakiongozwa na Balozi Egon Konchanke, viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na mashirika ya Maendeleo ya Kimataifa ya FZS, WWF, GIZ na KFW.Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Maghembe alisema ndege hiyo itasaidia jitihada za Serikali za kupambana na ujangili kwa kufanya doria katika anga ya Pori la Akiba la Selous na kusaidia kutoa taarifa za kiuhalifu pale itakapobainika na kuchukuliwa hatua stahiki za kukabiliana na uhalifu huo.

 “Ndege hii tunayoshuhudia mapokezi yake leo ni ukombozi kwa wanyamapori katika Pori hili la Akiba la Selous kwani itasaidia na kuimarisha doria za kupambana na ujangili ndani na kuzunguka eneo zima la hifadhi,” alisema Profesa Maghembe.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment