SIRI YA SIMBA KUTOA WACHEZAJI WENGI WA SOKA LA KULIPWA

Simba ni moja ya klabu kubwa na ya pili kuzaliwa mnamo 1936 hapa Tanzania baada ya Young African Sports 1935, ambayo kimsingi Simba imepata mafanikio makubwa kwa upande wa mashindano ya nje. Na hata michuano ya Kagame ni timu pekee iliyo chukua ubingwa mara nyingi

KWANINI SIMBA INATOA WACHEZAJI KUCHEZA SOKA LA KULIPWA?
1.Kuwapa thamani wachezaji wa timu B, uaminifu huwa unajenga kujiamini kwa mchezaji husika mara nyingi simba wanawatumia wachezaji wa kikosi B wanawapandisha na kucheza vizuri
2.Viongozi hubariki endapo mchezaji anatakiwa nje, mfano mzuri Emanuel Okwi,Waarabu walipo kuja kuhitaji huduma ya Okwi Simba hawakuwa wagumu na ukiangalia wakati ule ndio alikuwa tegemeo la timu kwa moyo mkunjufu walimuuza
Yanga waliweza kwa Shabani Nonda lakini huyo huyo mmoja tu ukilinganisha na Simba ambao sasa wanakula Pension yao Mbwana Samatta na Emanuel Okwi, huyu amechukuliwa na shujaa wetu kutoka Tanzania lakini alianzia Simba.


NINI KILII FANYA YANGA ISITOE WACHEZAJI?
Mimi na wewe hatukuwepo katika uongozi wakati wachezaji wa Yanga wako ON FIRE Mfano Waziri Mahadhi, Sekilojo Chambua, Salvatory Edward hawa walikuwa wa kimataifa. nini kiliwashinda? jamani nadhani uongozi haukuwa sawa kuwaruhusu. Mrisho Ngassa alipata nafasi lakini hakuweza kuitendea haki ilifika mahali kacheza dhidi ya Manchester United lakini alikataa dili la Timu kutoka Sudan yote hayo sio kwa viongozi.


NINI KIFANYIKE?
Tuna tatizo la uongozi Tanzania viongozi wakae sawa pia nidhamu za wachezaji kama Mbwana Samatta mathalani asingekuwa na nidhamu sidhani kama angefika alipo sasa. Nidhamu ,Nidhamu,Nidhamu yaan hii ndio nguzo ya mafanikio.
Tanzania huu ni wakati wetu kipengele cha Mbwana Samatta katika mkataba wake kinasema kila baada ya kipindi skauti wa Fc Genk watakuja kuangalia vipaji ili wavinunue,Sasa tupewe nini hapo?
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment