Bado
tunaendelea kuzihesabu stori za Bungeni, najua kuna watu wangu wanakosa
nafasi ya kutazama kupitia TV majumbani lakini mimi nahakikisha
nakusogezea kila linalonifikia ili na wewe ulipate. Bado Bunge la 11
linapitisha bajeti zinazombwa na Wizara.
Katika siki mbili za kujadili bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyoomba kutengewa kiasi cha Sh. 135,797,787,000 katika hotuba iliyowasilishwa na Waziri wake Jumanne Maghembe, Wabunge walipata nafasi pia ya kuchangia ambapo hapa nakukutanisha na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega …
>>’Wakati
mwingine hata mimi nashawishika kufikiria kwamba kabla hatujaingia
kwenye jengo hili tuwe tunapimwa kama tumevuta marijuana, katika hali ya
kawaida kijana hata kama umepigiwa kura na kuaminiwa na wananchi
ukaenda kutukana lazima utakuwa na tatizo kwenye akili yako‘
‘Jana yupo mwenzetu mmoja wa
kutoka Chama ninachotoka amezungumza mambo ya ajabu sana hapa, unaweza
kuona ni kwanamna gani watu hawaelewi ni nani katika nyumba hii ameingia
bila ya Chama kilichomleta. Wote tumezaliwa na vyama vyetu, hii
michezo haitaki hasira..! ‘
‘Watu
wa Dar es salaam bado wanatumia nishati ya mkaa, na Serikali inapiga
vita matumizi ya mkaa. Nimwambie Waziri nguvu tunayotumia kupiga vita
matumizi ya nishati hii, tutumie nguvu hiyohiyo kuhakikisha
tunawatafutia nishati mbadala Wananchi hawa‘
‘Tunawaambia watumie gesi
hata elimu yenyewe ya matumizi ya gesi inafahamika? matumizi ya gesi
hayakuanza leo, hata wasomi wenyewe wanaogopa kutumia gesi. Sasa tufanye
jitihada za kutoa elimu kabla ya kuwaambia wasitumie wasitumie..!‘
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment