Wabunge
wameitaka Ofisi ya Bunge iwaondolee mara moja utaratibu wa kusaini kwa
kutumia vidole mara mbili kwa siku kwa kuwa wao si wanafunzi.
Hoja
hiyo iliwasilishwa kwa njia ya mwongozo na kuungwa mkono na wabunge
wote isipokuwa mawaziri na Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji (CUF) mjini
Dodoma jana.
Katika
Mwongozo wake, mbunge huyo alisema kitendo cha kutakiwa kusaini mara
mbili kwa siku ni kero kwa wabunge na uonevu kwa kuwa hata Bunge
limekuwa likitumia muda wa mapumziko wa wabunge kwa kazi za Bunge.
“Mheshimiwa
Naibu Spika wewe mwenyewe muda mfupi umetangaza matangazo mbalimbali
yanayotaka baadhi ya wajumbe wa kamati wakutane baada ya saa saba
mchana, tunafanya kazi nje ya mapumziko yetu, haya haina tatizo...
“...tatizo langu ni kitendo cha wabunge kutakiwa kusaini mara mbili kwa
siku asubuhi na jioni, wakati mwingine tunatoka hapa saa saba, wabunge
tunashughulikia mambo mpaka saa 12, mbunge anatumia muda wake wa
mapumziko na ule wa kuhudhuria kikao cha jioni,” alisema Haji.
Alisema inasikitisha kuona mbunge anatolewa kwenye kazi za kujenga taifa ili aje tu asaini kwa kidole tena mara ya pili.
Alisema
jambo hilo linawatatiza wabunge kwa kuwa wanajiona kama wanachukuliwa
kama wanafunzi kwa kufuatiliwa kwani hata kwenye benki wafanyakazi
hawasaini na kufuatiliwa kama ilivyo kwa wabunge hao.
Alifafanua
kuwa kabla ya kuomba Mwongozo huo, alifanya utafiti kwenye benki
mbalimbali ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambao nao wana utaratibu
kama huo wa Bunge lakini hakuna mahali wanapotakiwa kusaini kwa vidole
mara mbili.
“Kutokana na uzito wa jambo hili naomba kutoa hoja wabunge mniunge mkono mpango huu ukome,” alisema na wabunge takribani wote walisimama ishara ya kumuunga mkono na kumpigia makofi na vigelegele.
Kwa
upande wake, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alisema kutokana na namna
wabunge hao walivyopokea suala hilo, pamoja na kwamba kikanuni jambo
hilo halikutakiwa kuombewa mwongozo bado litaangaliwa.
“Hata
hivyo, nifafanue kuwa kusaini mara mbili lengo lake si kuwafanya
wabunge wanafunzi, ila lengo ni kutaka kujua nani wapo humu ndani
(bungeni),” alisema Dk Ackson.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment