Abiria 10 Wahofiwa kufa maji, 20 Wanusurika

ABIRIA 10 kati ya abiria 30 waliokuwa wakisafiri kwenye boti wakitokea Mitomoni, wilaya ya Songea Vijinini, mkoani Ruvuma kwenda mnadani katika wilaya hiyo wanahofiwa kufa maji baada ya boti hiyo kuzama kwenye Mto Ruvuma.

Habari zilizopatikana jana mjini hapa zilieza kuwa, boti hiyo ilikuwa imejaza abiria pamoja na mizigo iliyokuwa ikipekwa kwenye mnada wa hadhara ambao upo jirani na kijiji cha Mitomoni mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Jitihada za kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa alikuwa ameungana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma kwenda kwenye eneo la tukio hilo.

Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Ruvuma, Hamis Kutiku, alisema Kamanda Mwombeji amekwenda kwenye eneo la tukio ili kujiridhisha ukweli wa tukio hilo.

Alisema taarifa kamili juu ya tukio hilo zitatolewa baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kufika eneo la tukio na kurudi mjini kwa ajili ya hatua zaidi kuchukuliwa.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment