Baada
ya kutangaza vita dhidi ya mashoga juzi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda jana alitangaza vita nyingine; hataki uvutaji shisha
akisema inachanganywa na vilevi vinavyoharibu vijana.
Makonda, ambaye alikuwa akihutubia Tamasha la Vijana lililoandaliwa na Upendo Media Group kwenye Uwanja wa Taifa aliagiza wavuta shisha hadharani, sigara na mashoga wakamatwe ndani ya siku saba.
Makonda, ambaye alikuwa akihutubia Tamasha la Vijana lililoandaliwa na Upendo Media Group kwenye Uwanja wa Taifa aliagiza wavuta shisha hadharani, sigara na mashoga wakamatwe ndani ya siku saba.
“Ni marufuku biashara ya shisha kwenye mkoa wangu. Wanaofanya bishara hiyo wote nitawakamata. Mimi ndiye mbabe wa vita,” alisema Makonda na kuongeza: “Nina
imani watakuwa wamefungasha virago vyao iwe ni kwenye klabu au baa
maana humo wanachanganya vitu vingi; bangi na vilevi ambavyo vina
madhara.”
Alisema
vijana wa vyuo na sekondari ndiyo waathirika wakubwa wa kilevi hicho,
ambacho huvutwa kwa njia ya bomba la mpira linalotoka kwenye jiko
maalumu ambalo tumbaku huunguzwa na kutoa moshi.
“Baada ya siku saba tutakutana (Gereza la Segerea),” alisema.
“Kwa
utafiti nilioufanya chini ya TFDA, shisha ina madhara makubwa kwa
wanaoivuta na wasiovuta. Inasababisha kansa ya mapafu na koo.
“Na pia inasababisha utegemezi ambapo mtu bila kuvuta hawezi kuona maisha, lakini pia inapunguza uwezo wa kufikiri na inamaliza nguvu kazi katika taifa,” aliongeza.
“Na pia inasababisha utegemezi ambapo mtu bila kuvuta hawezi kuona maisha, lakini pia inapunguza uwezo wa kufikiri na inamaliza nguvu kazi katika taifa,” aliongeza.
Kwa
mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kiwango cha shisha inayovutwa
kwa saa moja, ni sawa na kuvuta sigara kati ya 100 na 200.
Utafiti wa shirika hilo unaonyesha kuwa mvuta sigara wa kawaida huingiza nusu lita ya moshi kwa kila sigara, lakini mvuta shisha ni zaidi ya hivyo.
Utafiti wa shirika hilo unaonyesha kuwa mvuta sigara wa kawaida huingiza nusu lita ya moshi kwa kila sigara, lakini mvuta shisha ni zaidi ya hivyo.
Kuhusu
uvutaji wa sigara, Makonda alisema ndani ya siku saba zijazo ni
marufuku kuvuta sigara hadharani na kila anayehitaji kufanya hivyo
atapaswa kutafuta sehemu iliyojitenga ili akate kiu yake.
“Kila anayevuta sigara, atapaswa kuvuta sehemu ambayo hatawabughudhi wenzake.
"Tumechoka
kupanda magari na watu wanaovuta sigara, kukaa hoteli na watu wa aina
hiyo. Sasa mvutaji anapaswa kuvuta sehemu ya peke yake, na sio kwenye
jumuiko la watu. Madhara ni makubwa kwa tusiovuta kuliko wanaovuta,” alisema.
Maagizo
ya Makonda yanakuja ikiwa ni wiki moja tangu apige marufuku abiria na
dereva wa bodaboda kusafiria chombo hicho bila ya kuvaa kofia ngumu.
Alisema kupanda pikipiki bila kofia
hiyo ni dhamira ya kutaka kujiua kwa sababu dereva na abiria wakipata
ajali ni rahisi zaidi kupoteza maisha iwapo kichwa kitajipiga ardhini.
“Nimewasiliana
na kamati yangu ya usalama barabarani ya mkoa. Hili nitalisimamia
kikamilifu lazima wote wavae helmet na wakikamatwa wote watashtakiwa,” alisema.
Mapema
mwaka huu, mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Makonda alitoa
maagizo matatu yanayohusu ombaomba wa barabarani kuondoka na kubomolewa
kwa majengo makubwa yaliyojengwa kinyume na taratibu na yasiyo na
maegesho.
Agizo la tatu la Makonda lilikuwa ni wamiliki wa baa kutopiga muziki nje ya utaratibu wa vibali vyao.
Makonda pia alirudia wito wake wa kutaka watu wanaojishughulisha na biashara ya ushoga wakamatwe mara moja.
Alisema
miaka michache iliyopita Taifa lilikataa msaada wenye sharti la ushoga,
lakini inashangaza kuwa bado zipo taasisi zisizo za kiserikali
zilizoundwa kwa ajili ya kutoa misaada kwa watu wanaojihusisha na
vitendo hivyo.
“Nimefanya mazungumzo na Waziri
wa Katiba na Sheria. Hatutaki hili liendelee kwa sababu hiyo naiagiza
TCRA kuwa wapo watu wanaojitangaza kwenye instagram na vyombo vya habari
kwamba wao ni mashoga, wakamatwe haraka iwezekanavyo na kama kuna shoga
ana akaunti kwenye mitandao ya kijamii na wale wafuasi wake wote ni
watuhumiwa sawasawa na mhusika,” alisema.
Ushoga, ambao ni uhusiano wa mapenzi wa watu wa jinsia moja, ni marufuku nchini, kwa mujibu wa Sheria ya Adhabu.
Kwa
mujibu wa Sura ya 16, sehemu ya 154, mtu anayejihusisha na ngono na mtu
mwingine kinyume na maumbile au anayemruhusu mtu mwingine kufanya naye
ngono kinyume na maumbile, atakuwa amefanya kosa la jinai na kustahili
kifungo cha miaka 14 jela.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment