Jeshi
la Polisi jana walitumia mabomu ya machozi kurejesha hali ya amani
baada ya wananchi kuanza kupigana kwa sababu za kisiasa wakati
wakisherehekea ushindi wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein,
katika kijiji cha Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni, Pemba.
Mwenyekiti
wa CUF Wilaya ya Micheweni, Rashid Khalid Salim, alidai vurugu hizo
zimesababishwa na wanachama wa CCM kutoka katika kijiji cha Kwale
wilayani humo.
Alisema
baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) kutangaza matokeo ya
Uchaguzi Mkuu wa marudio, wanachama wa CCM katika kijiji cha Kwale,
walianza kukusanyika na ngoma zao na kuanza safari ya kuingia katika
kijiji cha Mjini Wingi, sehemu ambayo ni ngome ya wanachama wa CUF, huku
wakisherehekea kwa kurusha 'vijembe' (maneno ya kejeli) na matusi.
“Pamoja
na kutakiwa kuacha matusi wakati wakisherehekea ushindi wa Dk. Shein,
waliendelea na kusababisha wenzao kupandwa na ghadhabu kuwachemka na
kuanza kupigana,” alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema
baada ya kutokea vurugu hizo, wanachama wa CCM kutoka kijiji cha Kwale,
walilazimika kukimbilia Kituo cha Polisi Micheweni.
Alisema askari walipofika eneo la tukio, walianza kupiga mabomu ya kutoa machozi na kuvunja milango ya nyumba.
Mwenyekiti
huyo alisema nyumba 15 zilivunjwa milango wakati wakiwasaka watu
waliokuwa wakihusishwa na vurugu hizo ambazo zilianza kufanyika saa
10:00 jioni na kuendelea hadi usiku juzi.
Aidha,
alisema kwa mujibu wa mabaki ya milipuko, jumla ya mabomu 27 yanadaiwa
kupigwa mbali na nyumba kuvunjwa milango na kusababisha watu zaidi ya 28
kuyakimbia makazi yao katika kijiji hicho.
“Watu
wanne wamekamatwa akiwamo mtoto mwenye umri wa miaka 13, lakini
wananchi wengi wamekimbia makazi yao na kukimbilia katika kisiwa cha
Kojani na Maziwang'ombe,” alisema Rashid.
Hata
hivyo, alisema jambo la kushagaza polisi wameamua kuwakamata watu
waliofanyiwa fujo badala ya kuwakamata waliokuwa chanzo cha vurugu hizo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir, alithibitisha
kutokea kwa vurugu hizo na kwamba watu watano wanashikiliwa kwa
uchunguzi wa kuhusika na tukio hilo.
Hata
hivyo, alikanusha kuvunjwa milango 15 pamoja na kutumika mabomu 27
kurejesha hali ya utulivu baada ya wananchi kuanza kupigana.
Waliokamatwa
katika mkasa huo ni Kombo Khalfan Faki, Salim Hassan Khamis, Mjawiri
Faki, Khatib Dawa Juma na Assaa Bakar Ali, wakazi wa kijiji hicho.
Kwa
upande wake, Mkuu wa mkoa huo, Omar Khamis Othman, alisema hali katika
kijiji hicho imerejea kuwa ya kawaida na kuwataka wananchi kuendelea na
sherehe za kumpongeza Dk. Shein bila ya kuvunja sheria.
Alisema
wananchi waliokimbia makazi yao na kukimbilia katika kisiwa cha Kojani
na Maziwang'ombe, watakuwa ndiyo waliohusika na vurugu na kwamba raia
mwema hana sababu ya kukimbia askari.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment