April 6
mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Arusha mh. Daud Felix Ntibenda alitoa amri
ya kuyadhibiti makanisa ya kilokole jijini Arusha kwa madai kuwa
yanawasumbua wananchi kwa kupiga vinanda na kuimba usiku kucha.
Ntibenda alitoa amri hiyo ofisini kwake wakati akizungumza na wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wa mitaa yote ya jiji la Arusha.
Alisema hataweza kuvumilia makanisa hayo kuzinduliwa kila mahali katika makazi ya watu na kufanya ibada usiku kucha.
"Mimi
ni mkristo, sikatazi waumini kusali, lakini nataka kuwe na utaratibu
maalumu, sio kila kukicha unakuta kanisa jipya na kibaya zaidi
yanasumbua hata wageni wanaoingia jijini hapa." Alisema Ntibenda.
Kutokana
na kauli hiyo ya mkuu wa mkoa, Askofu Mkuu wa Kanisa na Ufufuo na
Uzima, Josephat Gwajima amejitokeza hadharani kupinga kauli hiyo.
Gwajima
amesema Tanzania ni nchi huru, na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania,
kila mtu ana haki ya kuabudu muda wowote na wakati wowote atakao bila
kuingiliwa na mtu yeyote.
Amesema
waumini wa makanisa ya kilokole Tanzania wako zaidi ya milioni 11,
hivyo kuwazuia kuabudu ni sawa na kutafuta matatizo mengine
Gwajima amesema waumini wa Kiislam huamka saa kumi usiku kuswali kwa sauti kubwa na hakuna mtu huwaingilia kwa kuwa hiyo ni haki yao kikatiba.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment