Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema hakuna
chama kilichokidhi matakwa ya kikatiba kutoa makamu wa kwanza wa Rais.
Rais Shein aliyasema
hayo jana alipokuwa akizungumza na Baraza la Wawakilishi visiwani
Zanzibar kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake kwa mara ya pili
kuongoza Umma wa Wazanzibar.
''Hakuna
Chama chama kinachokidhi kutoa makamu wa kwanza wa Rais huo ni uamuzi
wa wananchi na ni uamuzi wa kidemokrasia unaostahili kuheshimiwa ''Alisema Rais Shein.
Aidha Rais Shein katika hotuba yake kwa Baraza hipo pamoja na wananchi wa Zanzibar aliahidi
kuhakikisha Zanzibar inasonga mbele kimaendeleo kwa kujenga viwanda
maeneo mbalimbali na kuboresha huduma za kijamii pamoja na kupandisha
mishahara hadi kufikia shilingi laki 3 kwa kima cha chini.
Pia Rais Shein alisema
ataongoza Zanzibar kwa haki na watu wote ni lazima wafahamu kwamba yeye
ndiye Rais ambaye alichaguliwa kwa asilimia 91.4 hivyo uchaguzi haupo
tena hadi mwaka 2020.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment