Kafulila amesema anapinga ushindi wa Mbunge huyo nakuitaka Mahakama kupitia mawakili wake waruhusu kuhesabiwa kwa fomu namba 21B kutoka vituoni 382 fomu ambazo zilisainiwa na mawakala katika vituo vya jimbo lake.
Katika utetezi upande wa Kafulila ulitoa ushahidi kwamba alishinda kwa mujibu wa fomu ambazo zilisainiwa vituoni huku akiitaka mahamaka iiamuru serikali na mlalamikiwa watoe ushahidi wa fomu za matokeo zilizompa Mwilima ushindi ambapo mawakili wa serikali na Mbunge Mwilima wametaka kesi hiyo ifutwe.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 25 itakapoendelea tena ambapo Kafulila anawakilishwa na Profesa Abdallah Safari pamoja na Msomi Kagashe wakisaidiwa na wakili mwenyeji Daniel Lumenyera.
Upande wa mlalamikiwa, Hasna anawakilishwa na wakili msomi, Kennedy Fungamtama pamoja na mawakili wa serikali wanao mwakilisha Msimamizi wa Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ni washtakiwa katika kesi hiyo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment