Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka amesema hayo wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni katika Kata ya Dembetini, Jijini Arusha.Amewaambia wananchi mkoani hapa kwamba, Uchaguzi Mkuu umekwisha na sasa wana jukumu la kuweka kando masuala ya kisiasa, ili kila mmoja ajitume na kufanya kazi kwa bidii wakisubiri msimu mwingine wa siasa, mwaka 2020.
“Kila jambo na muda au wakati wake muafaka, wakati huu kuhubiri siasa, kumkosoa rais, mbunge au diwani si wakati wake. Kunyamaza kimya kuna thamani kubwa kama ya dhahabu na siyo kusema ovyo,” amesema.
Akirejea baadhi ya kauli za aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa za kumkosoa Rais Magufuli, Shaka amemtaka mwanasiasa huyo kukubali kuwa Dk. Magufuli anakubalika na sehemu kubwa ya Watanzania.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment