Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trickster, Sonobe Atsushi(kulia) akisoma taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).
Meneja Mradi kutoka Kampuni ya Afrika New Business Development Department, Alex Kapungu (kushoto) akiwa na Atsushi.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
KAMPUNI ya Kijapani inayofanya shughuli zake hapa nchini za kubadilisha fedha za kigeni pamoja na utengenezaji wa video za filamu ijulikanayo kama ‘Tricster’ imeandaa shindano la biashara litakalozishirikisha nchi tano za Afrika zikiwemo Kenya, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji wa mashindano hayo, Tanzania.
Mchakato wa shindano hilo tayari umeshaanza na mwisho wa shindano ni Julai, mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam wakati Meneja Mradi wa Kampuni ya Afrika New Business Development Department, Alex Kapungu ambao ndiyo wadhamini wa shindano hilo alipokuwa akizungumza na wanahabari.
Kapungu alieleza kuwa lengo la shindano hilo ni kusaidia kuboresha ujasiriamali katika Bara la Afrika na kuwawezesha wananchi kuingia katika soko la ajira hususan wanapokuwa wamebuni wazo na likakubalika huku akisema kwa hapa Tanzania ni kwa mara ya kwanza kufanyika, hivyo ni fursa nzuri kwa wajasiriamali na wale wanaotaka kuwa wajasiriamali kushiriki.
Alifafanua kuwa vigezo vya kushiriki shindano hilo mshiriki anatakiwa asiwe chini ya umri wa mika 18, ajue kuongea na kuandika lugha ya Kiingereza kwa ufasaha na kuwa na hati ya kusafiria.
Kapungu alitoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki ili wapate fursa ya kuanzisha biashara kwa njia ya mtandao kupitia mawazo watakayoyatoa ili kupanua wigo katika jamii.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trickster, Sonobe Atsushi, alisema washiriki watakaoingia nusu fainali watapata fursa ya kutembelea nchi ya Japan ambapo mshindi wa kwanza atapata pesa dola elfu tano za Kimarekani.

Na Denis Mtima/Gpl
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment