Kigogo Amnunulia KIIZA Gari!


kiiza mbwembweMshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza ‘Diego.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa Simba, Hamisi Kiiza ‘Diego’ anatarajia kupokea gari jipya kutoka kwa tajiri ambaye aliahidi kumpa kama zawadi iwapo angefikisha mabao 19 ya kufunga.
Kiiza kutoka Uganda sasa yuko kileleni kwa wafungaji bora akiwa na mabao 19 akifuatiwa na Mrundi, Amissi Tambwe wa Yanga mwenye 18 na tayari kigogo huyo yuko tayari kutimiza ahadi yake.

Habari za uhakika asilimia mia, zinaeleza kigogo huyo mpenzi mkubwa wa Simba, tayari ameagiza gari la Kiiza.
“Nimeambiwa ni Toyota, ila sijajua ni muundo upi lakini kuna wachezaji ambao wanamfurahisha jamaa, nimeambiwa ameagiza magari manne au matano. Hivyo kuna wachezaji wengine wa Simba watapata magari pia,” kilieleza chanzo.

“Huenda ndani ya wiki mbili au tatu, magari aliyoagiza kutoka Japan yatakuwa yametua Dar ila nimeambiwa kuna mchezaji mmoja katika safu ya ulinzi, mwingine nafikiri itakuwa katika safu ya kiungo. Hakika sijui ni kina nani lakini ameagiza magari yote.

“Lengo lake ni kuwashukuru wachezaji walioonyesha kujitolea lakini anafanya hivyo kwa mapenzi yake na si rahisi kumzuia au kumlazimisha.
“Unajua, hawezi kutoa magari kwa wachezaji wote lakini anacholenga hasa ni kuongeza motisha kwa ambao wamekuwa wakijituma na wanaoweza kubadilika waisaidie timu katika mechi zilizobaki za ligi, watafaidika pia,” kilifafanua zaidi chanzo.

Taarifa nyingine zilieleza kwamba kigogo huyo alitaka kumhamasisha Kiiza afunge zaidi na aliweka idadi ya mabao 19 kwa kuwa kwa kipindi kirefu sasa wafungaji bora wamekuwa wakiishia katika mabao 19 au chini ya hapo.

Mchezaji wa kwanza kupewa gari nchini hasa katika miaka ya 2000 alikuwa ni Juma Kaseja wakati alipopewa gari aina ya Toyota wakati akitokea Moro United na kujiunga na Simba mwishoni mwa mwaka 2002.
Baadaye ilikuwa ni kama ada wachezaji kupewa magari wakati wa usajili. Kiiza anakuwa wa kwanza kupewa gari kutokana na mabao aliyofunga katika kikosi chake.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment