Manispaa Ilala Yatafuna Mil 16


Valentino Mlowola, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na KUpambana na Rushwa (Takukuru)
MANISPAA ya Ilala jijini Dar es Salaam imetafuna jumla ya Sh. 16 Milioni kutoka kwenye miradi mbalimbali, anaandika Faki Sosi.
Edson Makallo, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Ilala amesema, pesa hizo zililenga kuingizwa kwenye Mfuko wa Dawa ‘Basket Fund.’

Makallo amesema ubadhirifu umefanywa na maofisa kwenye manispaa hiyo na kwamba, hatua za kisheria zitachukuliwa.

Hata hivyo amesema, Takukuru imefanikiwa kuokoa zaidi ya Sh. 104 milioni. Kati ya fedha hizo, Sh. 12 Mil zilidaiwa kuwa malipo ya malimbikozo ya mishahara ya walimu wa Shule za Msingi na Sh. 92 Milioni zilizodaiwa kutengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya St Mary’s, Tabata.

Amesema, barabara hiyo ilijengwa chini ya kiwango na kwamba, baada ya uchunguzi mkandarasi alirudisha fedha hizo na yeye (mkandarasi) kuingia hasara.

Ametaja maeneo yanayolalamikiwa na wananchi kwenye manispaa hio kuwa serikali za mitaa, mahakama, elimu, mawasiliano (Ttcl na Posta), polisi, maliasili, afya, taasisi za kifedha, Viwanada na Biashara, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Uhamiaji, Sekta binafsi na Chuo cha Ubaharia.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment