SIMBA SC Yafanyiwa Umafia na YANGA SC

amisMshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam IMEFAHAMIKA kuwa kiongozi mmoja wa wa Yanga ndiye amefanya umafia hadi sasa wachezaji wawili mastaa wa Simba, Hamis Kiiza na Juuko Murshid wameshindwa kuungana na timu hiyo.
Simba imekuwa kwenye kiwango kizuri sana kwa siku za hivi karibuni, hali ambayo imekuwa ikizitisha timu pinzani za Yanga na Azam.

Timu hiyo ambayo ndiyo kinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, sasa ipo kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Coastal Union, utakachezwa Aprili 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kama itashinda, basi itafuzu nusu fainali ya Kombe la FA.

Wachezaji hao wiki iliyopita walikuwa nchini Uganda kwa ajili ya kuitumikia timu yao ya taifa ‘The Cranes’ ilipocheza na Burkina Faso katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon), zitakazofanyika Gabon mwaka 2017, lakini hadi leo hawajatua nchini wakiwa wamezidisha siku sita.
juuko shangilia uraStaa wa Simba, Juuko Murshid.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, sababu kubwa inayosababisha wachezaji hao kushindwa kujiunga na kikosi hicho ni hujuma ambazo zinafanywa na kiongozi huyo wa Yanga.

Kikizungumza na Championi chanzo hicho kikiwa na uhakika wa hali ya juu kilisema kuwa:
“Kuna tatizo kubwa Simba kwa sasa, Kiiza na Juuko bado hawajarudi hapa nchini na hadi leo wameshazidisha siku sita tangu siku waliyokuwa wanatakiwa kurudi.
“Tuna taarifa zote kuwa kuna kiongozi mmoja wa Yanga ambaye siyo wa kuchaguliwa, lakini ana jukumu kubwa kwenye timu hiyo, amewaficha na yeye ndiye amekuwa akiwapa fedha kila siku na kuwataka waendelee kukaa hukohuko.

“Ameshamwambia Juuko kuwa anamtafutia timu nchini Lebanon na asirudi tena nchini kujiunga na Simba, lakini amekuwa akizungumza na wachezaji hao kwa kuwa ni mtu mkubwa wamekuwa wakimsikiliza.
“Lakini kwa kuwa uongozi umeshajua hujuma hizo na una ushahidi, hakika najua hawawezi kukaa kimya watatoa tamko kali sana,” kilisema chanzo hicho cha uhakika.

Hata hivyo, Championi jana ilipata taarifa kuwa uongozi wa timu hiyo utafanya mkutano na waandishi wa habari leo saa tano na kuna uwezekano wakazungumzia mambo hayo.
Uongozi wa timu hiyo haukupatikana kuzungumzia ishu hiyo.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment