Taswira ya Msiba wa Mwanamuziki NDANDA Kosovo Leo Jijini Dar [+PICHAZ]

NAPE NA MAKONDA MSIBANIWaziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) samabamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda wakiwa msibani hapo.KING DODOO AKIWEKA MAMBO SAWA
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Ndanda Kosovo, King Dodoo akiweka mambo sawa msibani.
KINGBLAISE WA FM AKADEMIA AKIIMBA KWA HUZUNI
King Blaise wa  FM Academia akiimba kwa huzuni.
MAMA YAKE NDANDA ANNE MARIE KOMBEMama  yake  Ndanda Anne  Mariane Kombe akilia kwa uchungu. MKE MWINGINE WA MAREHEM, INFRANCIE (1)Mke  wa pili wa  marehenu, Infrancie.
MMOJA WA WAKE ZA MAREHEM, FRANCIE AKICHEZA MUZIKI HUKU AKILIA KWENYE JENEZA BAADA YA SEBENE KUCHANGANYA
Francie  akilia mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mumewe.
MMOJA WA WAOMBOLEZAJI
Mmoja wa waombolezaji akilia kwa uchungu.
TOTOO ZEBINGWA AKIMSALIMIA NAPE
Totoo Zebingwa  akimsalimia  NAPE NA MAKONDA MSIBANI
WAZIRI wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda wamewaongoza mamia ya waombolezaji katika shughuli ya mazishi ya staa wa Muziki aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita, Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar,

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya mwanamuziki huyo, King Dodoo marehemu anatarajiwa kuzikwa leo Jumatano kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo maandalizi yamefanyika kwenye nyumba ya Ubalozi wa Congo DRC iliyopo Kinondoni-Hananasif jijini.

Dodoo alisema wameamua kumzika marehemu hapa nchini kufuatia wosia wake alioutoa mbele ya Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza na wanamuziki wa dansi katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni mwezi uliopita.
Katika kikao hicho Ndanda alisimama na kusema endapo akifa basi maiti yake izikwe hapa Tanzania kwa kuwa ndipo mahali alipopatia mafanikio makubwa ya kimuziki na anahisi ndiyo sehemu ambayo atazikwa na watu wengi kuliko Lubumbashi alikozaliwa.
PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment