Miongoni mwa habari kubwa za dunia hivi karibuni ni Nyaraka za Panama ‘Panama Papers‘ zilizofichua kashfa ya ukwepaji kodi na utakatishaji fedha ulikofanywa na viongozi wa mataifa mbalimbambali, watu maarufu na wanasiasa ambapo baada ya nyaraka hizo kuzidi kuwaumbua watu wakubwa duniani, Tanzania Takukuru wakasema itacheck kama kuna watanzania wamo kwenye list hiyo.
Inasemekana nyaraka hizo za Panama zilizovuja pia zilimtaja kiongozi na mwanzilishi wa kanisa Synagogue Church of All Nations ‘SCOAN’, T.B Joshua na mkewe Evelyn kwamba wanamiliki kampuni ya Chillon Consultancy Limited.
Tuhuma hizo zilianza kuchapishwa na mtandao wa habari wa Premium Times ambapo kupitia official page yake ya facebook T.B Joshua ameonya dhidi ya kauli za kumkashifu yeye na kanisa lake na kusisitiza kwamba yeye sio mfanyabiashara na hana hizo biashara.
TB Joshua amesema habari hizi zimeandikwa na Mwandishi wa habari ambaye wamekua hawaelewani toka jengo la kanisa hilo lianguke na kupoteza maisha ya watu, kutokana na kutoelewana huko TB Joshua amekua akipokea mfululizo wa habari mbaya zinazoandikwa na Mwandishi huyo wa habari.
"I have NOTHING to do with the #PanamaPapers." - TB Joshua
— TB Joshua (@SCOANTBJoshua) April 11, 2016
Please read T.B. Joshua's official statement here - https://t.co/euAqf2hNG1
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment