KAMBI
Rasmi ya Upinzani imepinga tabia ya ‘kutumbua majipu’ inayofanywa na
serikali ya Dk John Magufuli hivyo imewataka watumishi na watendaji wa
umma waliosimamishwa au kufukuzwa kazi na mawaziri, kufungua mashauri
Mahakama Kuu ya Tanzania ili kupinga kufukuzwa kwao na baadhi ya
mawaziri.
Hayo
yamesemwa leo katika hotuba ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu
Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Katiba
na Sheria kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
Kwa
mujibu wa hotuba hiyo, Lissu amesema kuwa baadhi ya mawaziri
waliosimamisha na au kufukuza kazi watumishi wa umma kwa jina maarufu
kutumbua majipu, walifanya maamuzi hayo kinyume cha sheria.
Ameongeza
kuwa Mawaziri hao hawakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kwa sababu
hawajakasimishwa mamlaka ya utekekelezaji wa majukumu yao kwa mujibu wa
kifungu cha sheria cha 5(1) cha utekelezaji wa majukumu ya kiuwaziri.
Kutokana
na hali hiyo kambi ya upinzani imesema watumishi wote ambao
wametumbuliwa wana haki na uwezo wa kwenda mahakamani na kuomba mahakama
kutengua utumbuaji wa majipu uliofanywa na mawaziri wasiokuwa na
mamlaka hayo kinyume cha sheria.
“Kambi
rasmi ya upinzani inaamini kuwa kwenda kwa watumishi hao mahakamani
hakutawasaidia pekee kupata haki zao, bali pia kutakomez a vitendo vya
kuendesha nchi kienyeji na bila kufuata sheria vinavyoelekea kushamiri
chini ya utawala wa Rais John Pombe Magufuli,” amesema Lissu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment