SNURA Akubali Yaishe... Awaomba Radhi Watanzania Kwa Video ya Chura

Mwimbaji wa muziki wa Mduara nchini Snura Mushi ameomba radhi kwa umma wa Watanzania kwa kosa la kutengeneza, kuzindua na kuweka mitandaoni video ya udhalilishaji wa mwanamke na isiyozingatia maadili ya Kitanzania ya muziki unaoitwa "Chura".

Akizungumza na vyombo vya habari leo Snura amesema wakati wa utayarishaji wa video hiyo mvua ilinyesha hivyo madansa walilowana.
"Baada ya kuona wamelowa ilibidi tusitishe kupeleka katika televisheni na kuiacha you tube, Snura hajafungiwa bali video yangu ilisitishwa na mimi nilizuiwa kujihusisha na sanaa mpaka nijisajili," amesema Snura.

Meneja wa mwanamuziki huyo Hemedi Kavu amesema tayari walishakwenda Basata tangu jana kuomba usajili, leo wamepatiwa cheti cha usajili.
"Tumeshajisajili Basata, pia tayari tumeshaitoa video hiyo kwenye mtandao wa YouTube, tumeshalitekeleza na akaunti ya wimbo huo imeshafutwa na tunatarajia kuifanya video hiyo upya," amesema Hemedi Kavu.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment