Wakati jeshi la polisi likisema linajiimarisha, vitendo vya ujambazi vinazidi kuitikisa nchi baada ya kundi
la watu wasiojulikana kuvamia ofisi za Kampuni ya Ahsante Tours ya mjini
Moshi, kuua walinzi wawili na kuiba Sh 65.5milioni.
Tukio hilo limekuja
siku chache baada ya watu wasiojulikana kuvunja duka la kubadilisha
fedha la Chase Forex Bureau De Change la mjini Moshi na kuiba zaidi ya
Sh120 milioni.
Mbali na tukio hilo, Juni 12 mwaka huu, watu watano
wakiwa na bunduki aina ya SMG, walivamia mji wa Magugu wilayani Babati
mkoani Manyara na kupora Sh2.5 milioni.
Tofauti na tukio hilo la Magugu,
hivi karibuni Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam waliwaua watu
watatu eneo la Masaki katika majibizano ya risasi na Polisi.
Ukiachilia
matukio hayo, taarifa kutoka mikoa mbalimbali nchini zinaonyesha uporaji
wa fedha na mali kwa kutumia pikipiki maarufu kama bodaboda, unazidi
kushika kasi maeneo mbalimbali.
Wengi wa wanaolengwa na wahalifu hao ni
wateja wanaotoka kuchukua pesa benki au wanaokwenda kuchukua fedha jambo
ambalo limezua hofu kuwa huenda baadhi ya wafanyakazi wa benki
wanashirikiana na wahalifu.
Lakini, tishio kubwa
zaidi la uhalifu linatokana na kuibuka kwa makundi ya kihalifu
yanayokuwa yamejihami kwa silaha za kivita, yakiwamo mabomu ya kurushwa
kwa mkono, yakichinja raia na kupora.
Hivi karibuni, Polisi Jijini Dar
es Salaam waliwaua watuhumiwa hatari wawili waliokuwa wamejihami kwa
bunduki na mabomu, wanaotuhumiwa kuchinja watu nane Jijini Tanga na
watatu Jijini Mwanza
Hali hii ndio imemsukuma Rais John Pombe Magufuli, kuwaagiza polisi kuhakikisha ‘wanawanyang’anya’ majambazi silaha haraka kabla ya kuwadhuru polisi ama raia wasio na hatia.
Hali hii ndio imemsukuma Rais John Pombe Magufuli, kuwaagiza polisi kuhakikisha ‘wanawanyang’anya’ majambazi silaha haraka kabla ya kuwadhuru polisi ama raia wasio na hatia.
Uporaji Ahsante Tours
Tukio la mauaji ya walinzi wawili ofisi za Ahsante Tours, lilitokea
usiku wa kuamkia jana, baada ya watu hao kuwazidi nguvu walinzi na
kuwafunga kamba kisha kuwapiga kwa kitu butu kichwani.
Kampuni hiyo
inamilikiwa na mfanyabiashara Cathbert Swai na mkewe Stella Shangali,
ambao pia wanamiliki hoteli ya kitalii ya Weruweru River Lodge iliyopo
Mailisita, nje kidogo ya mji wa Moshi.
Taarifa kutoka kwa baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni hiyo ambayo ni moja kati ya kampuni zinazoongoza
kwa kupokea watalii wengi, zinadai huenda tukio hilo ni mpango wa ndani.
“Kuna maswali mengi tunajiuliza. Walijuaje kuna kiasi hicho kikubwa cha
fedha kama taarifa hazikutoka miongoni mwetu?” alihoji mmoja wa
wafanyakazi aliyeomba jina lake lisitajwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, alisema kati ya
fedha zilizoibwa, kulikuwa na Dola za Marekani (Sh50
milioni) na Sh15 milioni za Tanzania.
Walinzi waliouawa wametajwa kuwa
ni Omar Mohamed (48), mkazi wa Matindigani Pasua na Dominick Cheddy
(41), mkazi wa Mailisita na wote ni wenyeji wa mkoa wa Tanga.
Kamanda
Mutafungwa alisema tukio hilo liligunduliwa saa 1.00 asubuhi na
wasamaria wema waliotoa taarifa polisi, na uchunguzi wa awali umebaini
watu hao walikata uzio wa ofisi hizo.
“Baada ya kuingia ndani ya jengo
hilo la ofisi walivunja ofisi ya meneja mkuu na baadaye ofisi ya mhasibu
ndio wakaiba Dola 23,300 na pesa za Tanzania Sh15 milioni,”alisema
Kamanda Mutafungwa.
“Tunashuku kuwa huenda hao majambazi waliamua kuwaua
hao walinzi baada ya hao walinzi kuwatambua. Bahati mbaya hawakuwa na
silaha yoyote hata panga hawakuwa nalo,”alisisitiza.
Kamanda Mutafungwa alisema Polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye inaonekana alikuwepo wakati mauaji na uporaji huo ukifanyika lakini, majambazi hao hawakumdhuru sehemu yoyote.
Kamanda Mutafungwa alisema Polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye inaonekana alikuwepo wakati mauaji na uporaji huo ukifanyika lakini, majambazi hao hawakumdhuru sehemu yoyote.
Hata hivyo, Kamanda Mutafungwa, aliwataka
wafanyabiashara kupeleka pesa benki badala ya kuzihifadhi ndani au
ofisini na kuwataka pia kuimarisha ulinzi ikiwamo kuweka CCCTV Camera.
Alitoa wito kwa wananchi wenye taarifa za waliohusika na tukio hilo,
kulisaidia Jeshi la Polisi kama ilivyotokea wiki moja iliyopita ambapo
taarifa zao zilisaidia kuwatia mbaroni wahalifu mbalimbali 30.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment