Mjamzito
mmoja, Magreth Charles (22), mkazi wa Kata ya Lyabukande Wilaya ya
Shinyanga amejifungulia kwenye korido la Kituo cha Afya cha Lyabukande
baada ya kukosa huduma kutoka kwa wauguzi.
Mjamzito
huyo alilazimika kujifungulia kwenye korido kutokana na wauguzi katika
kituo hicho kugoma kutoa msaada wakidai wako kwenye mapumziko na kumtaka
aende sehemu nyingine.
Mama
mkwe wa mjamzito huyo, Rachel Mpanda alisema walifika kituoni hapo
wakitokea kijiji cha Kizungu jirani na kituo hicho na walielezwa na mtu
waliyemkuta kuwa wauguzi wako mapumzikoni, hivyo hakutakuwa na huduma
yeyote.
“Baada
ya muda kidogo tukiwa tunatafuta namna ya kwenda kituo kingine, mwari
wangu alianza kusukuma mtoto, hivyo nikaamua kuomba msaada kwa
wapitanjia ili wamsaidie ajifungue, alifanikiwa kujifungua mtoto wa
kiume,” alisema Mpanda.
Diwani
wa kata hiyo, Joseph Misiri alisema tukio la mwanamke huyo kujifungua
kwenye korido si la kwanza na kwamba kuna mwanamke mwingine alikosa
huduma hiyo na kusababisha mtoto kufariki dunia.
“Serikali
haina budi kuwachukulia hatua wauguzi katika kituo hiki kwani
wanasababisha kupoteza maisha ya watoto wachanga, mwishowe watasababisha
kupoteza maisha kwa wajawazito kwa kukosa huduma ya matibabu,” alisema Misiri.
Mmoja
wa wauguzi katika kituo hicho, Zulfa Mussa alisema kituo hicho kina
watumishi watatu; muuguzi mmoja alikuwa amempeleka mgonjwa hospitali ya
rufaa, daktari mfawidhi wa kituo, Kadela Mashaka alikuwa semina na yeye
alikuwa zamu usiku, hivyo alitakiwa kupumika mchana huo.
“Kwa
kawaida aliyekuwa zamu ya usiku anatakiwa kwenda kupumzika kujiandaa na
zamu yake nyingine, hivyo niliondoka kituoni na kumwacha mtaalamu wa
maabara,” alisema Zulfa.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kiomoni Kibamba alipohojiwa alisema hana taarifa na kuahidi kufuatilia.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment