Waziri Mkuu Asisitiza Watanzania Kuendelea Kulinda Amani

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa wito kwa makundi mbalimbali nchini kuendelea kuilinda amani iliyopo nchini.
Ametoa kauli hiyo Jumatatu hii katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam katika sikukuu ya Eid.
“Waislamu wote, mashekhe, wanataaluma wote, na kila muislam popote alipo, tunalo jukumu kubwa sana la kuendelea kusisitiza uwepo wa amani na utulivu katika nchi yetu, jambo hili ni muhimu na litaendelea kutulinda na kumfanya kila mtanzania kufanya majukumu yake akiwa na uhakika kwamba ataamka asubuhi atarudi nyumbani atakuta familia yake wote wapo salama,” alisema.

Hivi karibuni pia Rais John Magufuli akiwa visiwani Pemba alisisitiza suala la amani kwenye hotuba yake.
BY: EMMY MWAIPOPO
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment