Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein akimuapisha Bwana Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar, hafla iliyofanyika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja..
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali
Mohamed Shein leo amemuapisha Bwana Said Hassan Said, kuwa Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar.
Wageni waliohudhuria kwenye hafla hiyo ya kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyeikiti wa
Baraza la Mapinduzi alimteua Bw. Said Hassan jana kushika wadhifa huo
kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 55 (1) cha Katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984.
Hafla ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu
huyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali
mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Miongoni mwao ni Jaji Mkuu wa Zanzibar
Mhe. Omar Othman Makungu, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis.
Wengine ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Hassan Othman Ngwali, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud
Mussa Wadi, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman
Khatib,Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment