Papa Francis Alivyoosha Miguu ya Wakimbizi, Alhamisi Kuu

Pope-francis-celebrates-foot-washing-1


Popa Francis alikubusu mguu wa mmoja wa wakimbizi hao
WAUMINI wa Kanisa Katoliki na Madhehebu mengine ya Kikristu kote duniani, juzi Alhamisi ilikuwa ni siku ya kuabudu Sakramenti ya Ekarist Takatifu ikiwa ni ishara ya kuanza kwa safari ya mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristu, Ibada ambayo kwa kawaida hufanyika matukio mbalimbali likiwemo la waumini kuoshwa miguu.

Katika tukio la waumini kuosha miguu, kiongozi wa ibada (padri, askofu, kardinali au papa) huchagua viongozi wa jumuiya, usharika, kigango, parokia au jimbo katika kanisam hilo kama wawakilishi wa waumini wengine na kuwaosha miguu yao kama ishara ya upendo kwao na kuwafuta makosa yao kama alivyofanya Yesu Kristu alipowaosha miguu mitume wake 12 kabla ya kula nao karamu ya mwisho ya Pasaka.

Juzi ilikuwa tofauti kwa Kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis baada ya kuamua kutembelea kituo kimoja cha wakimbizi kilichopo Castelnuovo di Porto, nje ya Mji wa Roma, kuwaosha miguu na kuibusi bila kujali itikadi ya dini zao. Wakimbizi hao walikuwa ni wa madhehebu ya Kiislam, Orthodox, hindu na wakatoliki. Papa aliosha miguu wanaume, wanawake na watoto.

Wakati akiiwasili kwenye kambi hiyo, Papa Francis alikaribishwa kwa mabango yaliyokuwa yameandkiwa kwa lugha tofauti yakimaanisha neno “Karibu”. Aliendesha ibada ya misa takatifu hapo ambayo ilihudhuriwa na maelfu ambao kati yao, watu 892 walikuwa ni wakimbizi waliohitaji hifadhi.

Wakimbizi hao walionesha kufurahishwa na kitendo cha Papa Francis kuwatembelea na kufanya nao ibada ya kuwaosha miguu huku wengine wakionekana kuchukua picha za na video za ukumbusho wa tukio hilo kuu duniani wakitumia simu zao za mkononi (smartphone).

Papa Francis hakusita kuelezea kuguswa kwake na namna ambavyo wakimbizi wanavyoteseka, safari yake ya kwenda Mexico anavyotumia muda wake mwingi kuwaombea wakimbizio hao ili wawe na amani na nchi zao ziondokane na machafuko.

Hii imekuwa tofauti kidogo na ilivyozoeleka kwamba sheria za kanisa kuwataka wachungaji kuwaosha miguu wanaume pekee, lakini Januari mwaka huu Papa Francis alibadili sheria hiyo ili kutoa nafasi kwa wanawake na mabinti kushiriki zoezi hilo duniani kote. Papa alianza kwa kuwaosha miguu na kuwabusu wanaume 12 akiashiria kama yesu alivyowafanyia mitume wake, baadaye papa aliwaosha.

Taarifa ya kutoka Makao Makuu ya Papa, Vatican Italia, imeeleza kuwa, Papa alichagua wanawake wanne na wanaume nane ambapo miongoni mwa wanawake hao ni raia wa Italia mmoja, Eritrea watatu. Wanaume walikuwa wakatoliki wanne raia wa Nigeria, Waislam watatu wa Mali, Syria na Pakistan na Mhindu mmoja wa India jambo ambalo halijawahai kutokea kwa kanisa katoliki.
Sheria hiyo mpya inaelekeza kuwa kila mtu ni ametoka kwa mungu, hivyo anahaki ya kutafakari mateso, kifo cha Yesu na kusherehekea ufufuko wake.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment