Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawen.
Dar es Salaam
HATIMAYE wakuu wa Mikoa yote
nchini wametii agizo la Rais John Magufuli lilokuwa linawataka wasilishe
ripoti ya idadi ya watumishi hewa kwenye mikoa husika.
Wakuu
hao wa mikoa wapya wamewasilisha ripoti za watumishi hao jana Jijini
Dar es Salaam kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, George Simbachawene ili kuchukuliwa hatua za kisheria
kwa watumishi waliohusika katika kashfa hizo.
Katika ripoti hizo zilizowasilishwa, Mkoa wa Mwanza unaongoza kuwa na watumishi hewa 334 ukifuatiwa na mkoa wa Arusha 270.
Mkoa wa Dar Es Salaam
Akiwasilisha ripoti ya watumishi hewa,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema katika mkoa wake
baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kamati mbali mbali
wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao watumishi hao hewa
wamepelekea serikali kupotea pesa zaidi ya Milioni 316 kwa mwaka mmoja.
“Katika mkoa huu tumepata
watumioshi hewa 73, ila wengi watahoji mkoa huu mkubwa kwa nini unakuwa
na watumishi hewa wachache, nataka kukwambia Waziri, bado tunaendelea na
uchunguzi wa kina,” alisema Makonda .
Mkoa wa Arusha
Kwa upande wake ,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daudi Felix Ntibenda alisema mkoa huo umegundurika kuwepo na watumishi hewa 270 ambao wamekuwa wakiisababishia hasara serikali ya Bilioni 1.8 kwa kipindi cha Mwaka mmoja,
Mkoa wa Dodoma
Pia Mkuu wa Dodoma Jordan Rugimbana alisema katika mkoa wake wamegundua kwenye mkoa huo una watumishi hewa 101 ambao amedai wameisabishia hasara serikali milioni 287.3 kwa kipindi cha miezi sita.
Mkoa wa Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
alisema katika mkoa wake wamegundua kuwa kuna watumishi hewa 15 ambapo
amemweleza Waziri Simbachawene kuwa licha ya hao, kuna watumishi 145
ambao hajaonana nao huku akidai kuwa akimaliza kuonana nao huenda idadi
ya watumishi hewa ikaongezeka.
Mkoa wa Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenelal
Mstaafu Salum Kijuu alisema mkoa wake wamebaini kuwepo kwa watumishi
hewa 14 ambao wamesababisha upotevu wa pesa za serikali Milioni 49.1
Mkoa wa Katavi
Pia Mkuu wa mkoa huu, Jeneral Raphael
Muhuga alisema mkuo huo umegundulika kuwepo kwa watumishi hewa 21 ambao
wameitia hasara serikali Milioni 20.7.
Mkoa wa Kigoma
Mkuu wa Mkuo huyo, Bregedia Jenaral Mstaafu Emmanuel Maganga alisema katika mkuo huo wamebaini kuwepo watumishi hewa 171 ambao wameitia hasara serikali milioni 114.6.
Mkoa wa Kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadick alisema wamebaini mkoa wake una watumishi hewa 111 ambao wameisababishia serikali hasara ya milini 281.4.
Mkoa wa Lindi
Kwa Upande wa Mkuu wa mkoa huo,Godfrey Zambi alisema mkoa wake unawatumishi hewa 57 ambao wameitia hasara serikali milini 36.2.
Mkoa wa Manyara
Kwa Upande wake mkuu wa mkoa huo,Joel
Bendera, alisema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 42 ambao wameitia
hasara serikali Milioni milioni 313.9.
Mkoa wa Mara
Kuhusu Mkuoa wa Mara,Mkuu wa mkoa
huo,Magesa Mulongo alisema katika mkoa wake wamebaini kuna watumishi
hewa 94 ambao wameitia hasara serikali milioni 121.
Mkoa wa Mbeya
Kwa upande wa Mkoa wa Mbeya,Mkuu wa
Mkuo huo,Amos Makalla alisema katika mkoa wake kumekuwa na watumishi
hewa 98 ambao pia wameitia hasara serikali Milioni 459 .6.
Mkoa wa Morogoro
Mkuu wa mkoa huo,Dkt Steven
Kebwe,ambapo alisema mkoa wake umegundulika kuwepo na watumishi hewa 122
ambao wameitia hasara serikali milioni 450.7.
Mkoa wa Mtwara
Mkuu wa mkoa huo, Halima Dendegu
amesema mkoa wake umebainikika kuwepo kwa watumishi hewa 17, huku
watumishi wengine 285 uchunguzi ukiendelea, ambapo watumishi hao 17
wameitia hasara serikali milioni 216.5.
Mkoa wa Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa John Mongella alisema mkoa wake umengundulika kuwa na watumishi hewa 334.
Mkoa wa Njombe
Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Dkt Rehema
Nchimbi alisema mkoa wake umekuwa na watumiwa na hewa 34 ambao amedai
wamekuwa wakiitia hasara serikali Milioni 20.1.
Mkoa wa Pwani
Mkuu wa Mkoa huyo,Mhandisi Evarist Ndikilo alisema Mkoa wake umekuwa na watumishi hewa 150 huku akishindwa kusema hasara ya fedha za serikali kwa madai kuwa uchunguzi unaendelea.
Mkua wa Rukwa
Mkuu wa mkoa huo,Kamishna Mstaafu
Zerote Steven alisema mkoa wake umekuwa na watumishi hewa, 18 na wametia
hasara serikali milioni 55.6.
Mkuo wa Ruvuma
Mkuu wa Mkoa huo,Thabiti Mwambungu alisema mkoa huo umekuwa na watumishi hewa 35 ambao wameitia hasara serikali milioni 58.4.
Mkoa wa Simiyu
Mkuu wa Mkoa huo,Antony Mataka alisema
mkoa huo umegundulika kuwa na watumishi hewa 62 ambao wameitia hasara
serikali ya Milioni 320.9.
Mkoa wa Singida
Mkuu wa mkoa wa huo,Mhandisi Methew
Mtigumwe alisema kuwa wafanyakazi hewa katika mkoa wake ni 231 na
kueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea ili kubaini zaidi.
Mkoa wa Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
alianisha kuwa katika mkoa wake watumishi hewa ni 48 ambapo wanaitia
hasara Serikali Milioni 118.7.
Mkoa wa Tanga
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela alisema kuwa watumishi hewa katika mkoa wake ni 104 ambapo alisema kuwa tathimini ya kuhakiki bado inaendelea.
Hata hivyo katika Mkoa wa Shinyanga
hali ilikuwa tofauti na mikoa mingine ambapo hadi sasa hakuna watumishi
hewa kutokana na mikakati iliyowekwa kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 na
mkuu wa mkoa aliyepita.
Pia, Mkoa wa Songwe hauna watumishi hewa kunatokana na kwamba mkoa huo ni mpya na mkuu wake wa mkoa ameapishwa wiki moja iliyopita.
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
[MATUSI HAYARUSIWI]
0 comments:
Post a Comment