Ulisikia Stori za IBRAHIMOVIC Kujiunga na ARSENAL? Wenger Katoa Majibu Kwenye Hii Video

March 18 baadhi ya mitandao ya soka barani Ulaya iliandika stori kuhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic kuwa yupo katika mipango ya kujiunga na klabu ya Arsenal ya Uingereza. 

Habari za Ibrahimovic kujiunga na Arsenal zilizidi kupata nguvu baada ya Arsenal ndani ya wiki moja kutolewa katika michuano Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA. Kabla ya kuelekea dhidi ya Everton, Arsene Wenger amesema ni kweli Ibrahimovic amekuwa na msimu mzuri na PSG, lakini sio vizuri kuanza kuwaza habari za usajili sasa hivi.
Sekunde 34 za Aresne Wenger kuhusu Zlatan Ibrahimovic
TUPE MAONI YAKO HAPO CHINI
[MATUSI HAYARUSIWI]
Share on Google Plus
    Facebook Comment
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment